Wakulima Wameshauriwa
Kutumia Teknolojia Mpya Ambazo
Zimekuwa Zikigunduliwa Na Kampuni Mbalimbali Za Kilimo Ili Kuongeza Mavuno kwa Kutumia vifaa Vinavyo tuzunguka.
Hayo Yamesemwa Na Mkufunzi Wa Kilimo
Kutoka Echo East Africa Bwana Herry Charles Wakati Wa
Utambulisho Wa Kifaa Kipya Cha Kupandia
Kiitwacho Maresha Planter Kinacho Panda Shamba Kwa Njia Ya Kukokotwa Na Ng’ombe.
Charles Amesema Teknojia
hii mpya ya Kupandia imekuwa na Faida mbalimbali “Faida
ya Kipandio Hiki Kinaotesha Vizuri Bila Kubananisha Mahindi , Maharage Pamoja Na Mazao Mengine Shambani Na Nikifaa Kizuri
Sana Na Kinatumia Muda Mfupi Wakati Wa
Kuotesha Ina Uwezo Wa Kupandia Heka Nyingi
Kuliko Kutumia Jembe Letu Ambalo
Linaotesha Eneo Dogo Kwa Masaa Mengi
Kuliko Maresha Planter”.
Afisa Kilimo kutoka
Kijiji cha Losikito Kata ya Mwandeti Meshack Luambano amesema kijiji cha Losikito
ni Kijiji cha Kwanza kuanza kutumia Kifaa hiki na kilianza kutumika kwa ufanisi
mkubwa na kufanikiwa kuleta matokeo kwa Baadhi ya wakulia ambao waliweza
kununua kipandio Hiki.
“Tunatamani
kutumia mikutano, Minada, Maonyesho ya Wakulima Nanenane na Vikundi mbalimbli ili kuweza kutangaza Kipandio hiki kipya ikiwa
ni Teknoljia ambayo inamsaidia na
kumrahisishia mkulima kupanda kwa Muda
mfupi na kuongeza Mavuno huku ikiwa ni
faida katika kuhidhi na Kutunza unyevuvu kwaajili ya Mbegu”Alisema Afisa
Kilimo Meshack Luambano.
Akibainisha Mafanikio
ambayo wameweza kuyapata tangu Teknoljia hii mpya imeanza kutumika ikiwa ni
Mwaka Mmoja (1) na Miezi mitano (5) Afisa Kilimo Luambano amebainisha Kuwa kwa
wakulima ambao wamekuwa wakiotesha kwa Ukanda wa Kiangazi kuanzia Mwezi wa Nane
(8) Kipandio Hiki kimekuwa na faida kubwa kwao kwani kimekuwa kikihifadhi Mbegu katika unyevu kwa umbali wa
Nnchi mbili (2) chini ya Ardhi hali ambayo inafanya mbegu isiliwe na ndege au
kwale na hata wanyama wengine.
“Mkulima
anaweza kuotesha mazao yake kwa siku moja (1) kuanzia Heka Tatu (3) mpaka (4) kutegemeana na
uweza wa Ngo’mbe na hali ya hewa kama jua limetoka au halijatoka lakini Mkulima
anashauliwa kupanda asubuhi kuanzia saa Kumi na Mbili Jioni 06pm”.
Alisema afisa Kilimo Luambano.
Baadhi Ya Wakulima
ambao wamekuwa wakitumia Kifaa hicho kwaajili ya Kupandia Kutoka Kijiji cha Losikito Mkoani Arusha
Wamesema Namna Ya Kutumia Maresho Planter Wakati Wa Kuotesha Shamba Na Pia Faida Wanazo
Pata Wakitumia Maresha Planter.
Pia Baadhi Ya Wafungaji
Wameeleza Wanafundishaje Ng’ombe Wakati Wakupanda Wakitumia Maresha Planter
Ili Mahindi, Maharage Pamoja Na Mazao Mengine
Yasichanganyike.
Hata Hivyo Afisa Kilimo
Bwana Benjamini Luambana Ametoa Hamasa Kwa Wakulima Wanunue Kifaa Hiki Cha Maresha Planter Kwasababu Kina
Faida katika kukuza sekta ya kilimo na kutumia
mfumo ikolojia kufuatia Kipandio Hiki Kutumia vifaa vinavyo tuzunguka.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Herry Charles
Huduma : Mkufunzi
Mahali : Arusha | Ngaramtoni
Kampuni : Echo East Africa
Contact : +255 784 97 01 99
+255 769 33 48 56
No comments:
Post a Comment