Mradi  wa  kilimo endelevu  plus  umezinduliwa  Jijini Arusha ukiwa na lengo la kukuza kilimo na kuchochea mfumo wa upatikanaji wa chakula kwa wakulima. 

Akizindua mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amesema Mradi huo utasaidia  Taifa kuwa na uzalishaji wa chakula cha kutosha utakaochangia jamii kuwa na Afya bora.

Mkurugenzi wa island of peace (IDP) Ayesiga Buberwa Hiza amesema mradi huo utachangia utunzaji wa mazingira kwa kutumia kilimo ikolojia.

Kwa upande wake Afisa Kilimo Mkoa Arusha Rosemary Masawe amewapongeza wadau walioanzisha mradi huo kwa kuleta fursa na manufaa kwa wakulima wadogo. 

Mradi wa kilimo endelevu Arusha plus Utafanyika kwa miak mitatu (3) huku ikilenga Vijana, wanawake na wakulima wa Vijijini.

Pia Mradi utasaidia kuanzisha Bustani Mashuleni na Kutoa elimu Mashuleni juu ya lishe  na uzalishaji wa mfumo wa Chakula endelevu mashuleni.

Inaelezwa kuwa Utekelezaji wa Mradi huo utaimarishwa na kusimamiwa kikamilifu na  Island of peace (IDP), RECODA na MVIWARUSHA katika wilaya mbili za mkoa wa Arusha.

“KILIMO ENDELEVU ARUSHA PLUS” KULETA AHUEWENI KWA WAKULIMA WADOGOWADOGO

No comments:

Post a Comment