MBEGU ZA ASILI ZILINDWE ZISIPOTEZWA NA ONGEZEKO LA MBEGU ZA KISASA : MVIWAARUSHA

 

 


Serikali kupitia wizara ya kilimo Imeombwa kutengeneza sera itakayo hamasisha wakulima wa mazao mbalimbali kulima na kuhifadhi mbegu za asili ili kuzitunza zisipotee katika ramani ya Kilimo.

 

Ombi hilo limetolewa na wadau wa kilimo mkoani Arusha katika maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani maadhimisho yaliyo Ratibiwa na Mtandao wa Vikundi vya wakulima mkoani arusha (MVIWAARUSHA) ambayo yalifanyika  mkoani Arusha.

 

Gabriel Mwalabwi ni Mwenyekiti wa Mtandao wa vikundi vya wakulima Ekenywa amesema kuwa mbegu za asili ni mbegu ambazo zilikuwa zikitumiwa na mababu na mabibi na kwa kipindi hicho hakukuwa na Magonjwa mbalimbali ukilinganisha na hivi sasa ambapo magonjwa kwa mimea yameongezeka.

 

"Mbegu za asili tangu zamani zilivyo kuwa zikitumika zilikuwa hazina Magonjwa zinapo kuwa shambani tofauti na hivi sasa ambapo kwenye mbegu za kisasa tunaona kumekuwa na magonjwa Mengi hivyo tunaomba serikali kupitia wizara ya afya waweze kuweka sera ambayo itasaidia kulinda mbegu hizi za asili" Gabriel Mwalabwi Mwenyekiti  wa Mtandao wa Vikundi vya wakulima.


 Juliana Simon ni Mkulima kutoka mkoani Arusha ambaye amekuwa akitumia  mbegu za asili ambazo anasema kwa sehemu kubwa zimesahaulika kutunzwa huku akitolea mfano juu ya mbegu zilizo sahaulikaza Nyanya.  

 

"Zamani kulikuwa na Nyanya ndogondogo ambazo walizita nyny mshenzi lakini pia kulikuwa na nyanya ambazo zilikuwa zinajiotea na zilikuwa zina kaa muda mrefu bila kuoza tofauti na hizi sasa ambapo nyanya zinakaa muda mfupi tu zimeoza''   Alisema Juliana Saimoni Mkulima  ambaye amekuwa akitumia mbegu za asili.        


 Akitolea Majibu kuhusu utunzaji na Uhifadhi wa Mbegu za asili  kwa upande wa serikali katika maadhimisho ya siku  chakula  Duniani afisa kilimo mkoa wa Arusha Rose Moses amesema  serikali imekuwa ikiwashauli wakulima kutumia mbegu za asili kulingana na Jogrofia ya maeneo kwani kuna baadhi ya maeneo ambayo  mvua zipo chini ya wastani na mbegu.

 

Mbegu za asili ni muhimu kwa sababu zinaweza kusaidia kuendeleza kilimo cha kiasili, ambacho hakitegemei mbegu za kisasa au kemikali nyingi. Pia, zinaweza kusaidia katika kuhifadhi uhai wa mimea na viumbe vinavyotegemea mimea hiyo.

 

Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Tanzania wanafanya juhudi za kuendeleza na kuhifadhi mbegu hizi, ikiwemo kuanzisha vituo vya kuhifadhia mbegu na kutoa elimu kwa wakulima kuhusu umuhimu wa kutumia mbegu za asili.

No comments:

Post a Comment