Wakristo wametakiwa kumuabu Mungu katika Roho na Kweli Badala ya kuamini katika dini  kuwa  ni Mpango wa Mungu katika Kumuabudu.

 

Akihubiri katika Ibada ya Jumapili Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Naivera Church Apostolic Tanzania Lililopo Arusha  Bishop Dkt Julius Laizer amesema Kumuabudu Mungu kuna anza na Mtu ambaye Ameokoka.

 

Amesema Mkristo hawezi kumuabudu Mungu katika Roho na Kweli kama hajaokoka  kwani Yesu ndiye amepewa Mamlaka na Mungu ya Kutawala Dunia na Vitu vyote Vilivyopo ndani Yake.

 

Aidha amebainisha kuwa kuokoka sio Dini Mpya Kuokoka ni kuzaliwa mara ya Pili kwani kuzaliwa mara ya kwanza ni kile kipindi ambacho  mwanadamu anazaliwa kutoka Tumboni mwa Mama yake. 

 

Hata hivyo Sanjari na Hilo Bishop Laizer ameeleza kuwa Wokovo ni Malango wa kumfungulia Mtu  njia ya Kuanza Kumuabudu katika Roho na Kweli.


 

 CHANZO CHA HABARI

Jina : Bishop Dkt.Julius Laizer

Huduma : Naivera Church Apostolic

Mahali  : Arusha

Mamlaka : NCA

Contact : +255 74436865

 

BISHOP LAIZER : KUABUDU KATIKA ROHO NA KWELI KUNAANZA NA MTU ALIYE OKOKA


 

Wananchi waliothirika na mafuriko Arumeru na Karatu wamepatiwa msaada na Kanisa la new life pryer center chini ya mchungaji Ezekiel Odero Mombasa nchini Kenya.

 

Kanisa hilo limetoa kiasi cha Tsh Milioni 50 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko.

 

Akizungumza mara baada ya kufika katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda Mchungaji Ezekiel Odero amesema kuwa Tanzania ni nyumbani hivyo kupitia huduma ya Mungu anayofanya ni vyema kuwajali wale ambao wamepatwa na majanga hayo.

PASTOR EZEKIEL ATOA MILIONI 50 KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MKOANI ARUSHA

 

 


 Askofu wa kanisa la FPCT Tanzania Mch. Stevie Mulenga amewataka wafanyakazi wa Taasisi zinazosimamiwa na kanisa hilo kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuendelea kujenga mwili wa Yesu Kristo.

Askofu Mulenga ameyasema hayo katika ziara ya kutembelea taasisi za kanisa hilo zilizopo Jijini Arusha ambapo amepokelewa na viongozi na wafanyakazi ikiwemo Habari Maalum Media, Idara ya Maandiko Kimahama na Chuo cha Habari Maalum.

Akizungumzia  mafanikio na mipango ya kituo cha Habari Maalum Media Mkurugenzi Yusto Swai  ameshukuru kwa ujio wa Kiongozi huyo  na kuwatia moyo katika utendaji wao wa kazi  ambapo amesema kuwa wameweza kufikisha injili kwa watu wote kupitia vipindi vya redio na Tv.

Kwa upande wa wafanyakazi pamoja na viongozi wa taasisi hizo wamepokea maangizo ya askofu wao na kuahidi kufanya kazi kwa bidii kwa ushirikiano.

ASKOFU MULENGA : TAASISI ZIFANYE KAZI KWA USHIRIKIANO TUTAONA MATOKEO