Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na ustawi wa wanyama nchini Tanzania—ASPA—limekutana na waandishi wa habari jijini Arusha kujadili mbinu bora za kukabiliana na tatizo la upotevu wa punda katika maeneo ya mipakani, hususan mpakani mwa Tanzania na Kenya.
Shirika hilo limeeleza kuwa punda wameendelea kupotea kwa kasi, jambo linalodaiwa kusababishwa na biashara haramu ya mifugo na ukosefu wa udhibiti wa mipaka.
Katika mkutano huo, ASPA imeeleza kuwa punda ni miongoni mwa wanyama muhimu wanaotegemewa na jamii nyingi kwa shughuli za usafirishaji na uzalishaji, hivyo upotevu wao una athari kubwa za kiuchumi na kijamii.
Gladness Msemo, Afisa Elimu wa ASPA, amesema kuwa shirika hilo limekuwa likifanya utafiti katika maeneo mbalimbali ya mipakani na kubaini kuwa idadi ya punda wanaopotea imeongezeka kwa kiwango kinachotia wasiwasi.
"Tumeona ongezeko la matukio ya punda kupotea, hasa katika vijiji vilivyo jirani na mpaka wa Kenya. Hii ina madhara makubwa kwa wananchi wanaowategemea punda kwa shughuli zao za kila siku. Tunatoa wito kwa jamii kutoa taarifa mapema na kushirikiana katika kuwalinda wanyama hawa.”Gladness Msemo, Afisa Elimu ASPA.
Kwa upande wake, Robert Mbwambo, Afisa Ustawi wa Jamii wa ASPA, amesema shirika hilo limeandaa mapendekezo ya hatua za kuchukua ili kukomesha tatizo hilo.
Amesema hatua zinazopendekezwa zinajumuisha kuimarisha ufuatiliaji wa mifugo, kushirikiana na mamlaka za mipakani, na kutoa elimu kwa jamii.
"Tunataka kuona mfumo madhubuti wa ufuatiliaji wa punda mipakani, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa vikundi vya ulinzi shirikishi na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara. Punda hawa ni sehemu ya uchumi wa wananchi, hivyo jukumu la kuwalinda linapaswa kushirikisha kila mdau.”Robert Mbwambo, Afisa Ustawi wa Jamii ASPA.
Mwandishi wa habari Pendo Mkonyi amesifu hatua ya ASPA na kusisitiza jukumu la vyombo vya habari katika kuibua changamoto zinazohusiana na ustawi wa wanyama.
"Vyombo vya habari vinapaswa kuwa mstari wa mbele kuhabarisha jamii na kufuatilia kwa ukaribu matatizo kama haya. Upotevu wa punda si suala la kifamilia tu, ni suala la kijamii linalohitaji ushirikiano wa wadau wote.” Pendo Mkonyi, Mwandishi wa Habari.
ASPA imeahidi kuendelea kufanya tafiti, kutoa elimu na kushirikiana na serikali pamoja na jamii katika kukabiliana na tatizo la upotevu wa punda, ili kuhakikisha wanyama hao wanaendelea kulindwa na kutumika kama rasilimali muhimu kwa maendeleo ya wananchi.
UFUGAAJI : (ASPA) WAJA NA MKAKATI MPYA KUKABILIANA NA UPOTEVU WA PUNDA MIPAKANI
Arusha
Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre—ALMC—chini ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, imeweka historia mpya katika safari ya kuboresha huduma kwa watoto njiti na wale wanaozaliwa kabla ya muda kwa kuingia makubaliano na ICHA taasisi ya Mtoto Africa ili kuendeleza na kuboresha huduma hiyo ndani ya hospital hiyo.
Akizungumza baada ya makabidhiano hayo Mkurugenzi mtendaji wa hospital ya ALMC MKOANI Arusha Godwill Kivuyo amesema huduma hii itasaidi kila mtoto anaye zaliwa kupata nafasi ya kuishi hata kama atazaliwa kabla ya Muda wake.
“Ushirikiano huu mpya kati ya ALMC na ICHA—Taasisi ya Afya ya Mtoto Afrika kutoka Marekani—unafungua ukurasa mpya wa matumaini. Tunataka kuhakikisha kila mtoto anayejaaliwa kuzaliwa hapa, awe na nafasi bora ya kuishi na kukua katika mazingira salama.”
Daktari Stephen Swanson ni Mratibu wa Taasisi ya mtoto Africa (ICHA) amesema Kwa muda mrefu, changamoto za vifaa, wataalamu na teknolojia ya kisasa zimekuwa kikwazo kwa vitengo vya watoto njiti katika hospitali nyingi za Tanzania Lakini kupitia makubaliano haya mapya, safari ya mabadiliko imeanza rasmi.
“ICHA inajivunia kushirikiana na ALMC kwa sababu tunaamini katika uwezo wao. Lengo letu ni kuleta utaalamu, mafunzo, na vifaa vinavyoweza kubadilisha kabisa huduma za neonatal. Watoto hawa ni wadogo, lakini matumaini yao ni makubwa.”
Aidha Daktari wa watoto Dkt. Eunice Msuya ambaye amekuwa akihusika na watoto njiti katika hospital hiyo amebainisha namna ambavyo ushirikiano huo unatarajiwa kuwa kitovu cha huduma za kiwango cha juu, si tu kwa Arusha bali kwa Kanda nzima ya Kaskazini na Africa.
“Hawa ni watoto wanaohitaji uangalizi wa karibu, ujuzi wa hali ya juu, na vifaa mahususi. Usimamizi sahihi katika dakika na saa za kwanza baada ya kuzaliwa huamua maisha yao. Tuna shukrani kubwa kwa programu hii ambayo itaongeza uwezo wetu wa kutibu na kuokoa maisha Wengi zaidi.”
Utafiti wa “Neonatal and Infant Mortality Risk” nchini Tanzania ulionesha kuwa watoto ambao wamezaliwa kabla ya muda wana hatari kubwa ya kifo kwani wanaweza kukabiliana na matatizo kama kupumua, kuzuia baridi , maambukizi, na shida za kukua baadaye hatua hii mpya ya ALMC na ICHA wanaandika hadithi ya matumaini hadithi ya ushirikiano itakayo saidia kupunguza Vifo vya watoto Njiti.
AFYA: MAKUBALIANO YA (ALMC) HOSPITAL ARUSHA NA (ICHA) KUBORESHA HUDUMA ZA MTOTO NJITI TANZANIA NA AFRICA KWA UJUMLA
Mamlaka ya Bima Tanzania Kanda ya kaskazini (TIRA) imewahimiza wazazi na walezi kuwakatia watoto Bima ya Afya na Bima Ya Maisha ili Mtoto kusaidika pale wazazi wanapo kuwa wamekumbwa na majanga mbalimbali ikiwemo kupoteza Maisha kwa kusomeshwa na Bima hadi Anapo hitimu elimu ya Juu.
Hayo Yamesemwa na Afisa Elimu kutoka Mamlaka ya Bima Tanzania Karo Modest mara Baada ya Kuhitimisha Bonanza lililofanyika Viwanja vya Shule ya Sekondari Ilboru mkoani Arusha na Kuwa na kukutanisha Klabu za Bima kutoka Shule za Arusha Dc bonanza lililokuwa na lengo la kutoa elimu juu ya Umuhimu wa Bima kwa mtoto.
Bonanza hilo Lilihusisha Klabu 36 kutoka shule mbalimbali zilizopo Wilaya ya Arusha Dc huku Mwenyekiti wa Klabu na Bonanza hilo Bi Upendo Mwakasata ambaye pia ni mwalimu Kiserian Sekondari akibainisha kuwa Bonanza hilo litaleta hamasa kwa Wazazi na walezi kuwakatia Bima watoto wao hususani Bima ya Maisha.
Aidha baadhi ya wanafunzi walio
jitokeza kushiriki katika katika Bonanza hilo wamesema Bonanza hilo
limeleta hamsa kwa wanafunzi na kujenga uelewa kuhusu nini Ambacho Bima
inafanya hususani kwa watoto walioko Shuleni kuanzia ngazi ya Msingi na
Sekondari
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima
Tanzania (TIRA), chini ya Sheria ya Bima Na.10 ya mwaka 2009, ni taasisi
ya serikali ilioanzishwa ili kutekeleza majukumu ya kusimamia soko na
kuendeleza biashara ya bima nchini na masuala yanayohusiana na bima kwa
mujibu wa sheria ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(TIRA) KANDA YA KASKAZINI YAFANYA BONANZA KUHIMIZA WAZAZI NA WALEZI KUWAKATIA WATOTO BIMA YA AFYA NA MAISHA

Shirika la Blue Cross Society of Tanzania linalojihusisha na Masuala ya kupinga ukatili na Madawa ya Kulevya limekabidhi mtaji kwa Wanawake ishirini (20) wahanga wa masuala ya ukatili mkoani Arusha lengo likiwa ni kuwainua na kuwawezesha kiuchumi.
Akikabidhi hundi ya Milioni sita Mkurugenzi Shirika la Blue Cross Society of Tanzania kutoka jijini Arusha Levokatus Nginila ameeleza kuwa dhumuni la kutoa kiasi hicho fedha ni kuwasaidia kuondokana na Utegemezi na kuboresha maisha yao.
Sambamba na hayo nae afisa mradi kutoka shirika ilo ameeleza lengo la kuwapo kwa mgao huo wa hundi ya shilingi milioni sita na laki mbili ni kwamba wamelenga huitaji wa watu wengi katikia jamii hususani wale walio athirika na dawa za kulevya.
Nao baadhi ya wanufaika wa fedha izo wamelishukuru shirika la msalaba wa blue kwa sapoti ya kiasi icho cha fedha kwani itawasaidi kuinua familia zao na kuendesha familia pasi na kikwazo
Inaelezwa kuwa Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayoleta msaada kwa wanawake wanaoishi katika mazingira magumu Tanzania yana nafasi kubwa katika kuboresha maisha ya wanawake wanao athirika na Ukatili.
NGOS SAIDIENI JAMII MSTUMIE RUZUKU KWA MASLAHI YA KWENU BINAFSI : BLUE CROSS SOCIETY
Serikali kupitia wizara ya kilimo Imeombwa kutengeneza sera itakayo hamasisha wakulima wa mazao mbalimbali kulima na kuhifadhi mbegu za asili ili kuzitunza zisipotee katika ramani ya Kilimo.
Ombi hilo limetolewa na wadau wa kilimo mkoani Arusha katika maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani maadhimisho yaliyo Ratibiwa na Mtandao wa Vikundi vya wakulima mkoani arusha (MVIWAARUSHA) ambayo yalifanyika mkoani Arusha.
Gabriel Mwalabwi ni Mwenyekiti wa Mtandao wa vikundi vya wakulima Ekenywa amesema kuwa mbegu za asili ni mbegu ambazo zilikuwa zikitumiwa na mababu na mabibi na kwa kipindi hicho hakukuwa na Magonjwa mbalimbali ukilinganisha na hivi sasa ambapo magonjwa kwa mimea yameongezeka.
"Mbegu za asili tangu zamani zilivyo kuwa zikitumika zilikuwa hazina Magonjwa zinapo kuwa shambani tofauti na hivi sasa ambapo kwenye mbegu za kisasa tunaona kumekuwa na magonjwa Mengi hivyo tunaomba serikali kupitia wizara ya afya waweze kuweka sera ambayo itasaidia kulinda mbegu hizi za asili" Gabriel Mwalabwi Mwenyekiti wa Mtandao wa Vikundi vya wakulima.
Juliana Simon ni Mkulima kutoka mkoani Arusha ambaye amekuwa akitumia mbegu za asili ambazo anasema kwa sehemu kubwa zimesahaulika kutunzwa huku akitolea mfano juu ya mbegu zilizo sahaulikaza Nyanya.
"Zamani kulikuwa na Nyanya ndogondogo ambazo walizita nyny mshenzi lakini pia kulikuwa na nyanya ambazo zilikuwa zinajiotea na zilikuwa zina kaa muda mrefu bila kuoza tofauti na hizi sasa ambapo nyanya zinakaa muda mfupi tu zimeoza'' Alisema Juliana Saimoni Mkulima ambaye amekuwa akitumia mbegu za asili.
Akitolea Majibu kuhusu utunzaji na Uhifadhi wa Mbegu za asili kwa upande wa serikali katika maadhimisho ya siku chakula Duniani afisa kilimo mkoa wa Arusha Rose Moses amesema serikali imekuwa ikiwashauli wakulima kutumia mbegu za asili kulingana na Jogrofia ya maeneo kwani kuna baadhi ya maeneo ambayo mvua zipo chini ya wastani na mbegu.
Mbegu za asili ni muhimu kwa sababu zinaweza kusaidia kuendeleza kilimo cha kiasili, ambacho hakitegemei mbegu za kisasa au kemikali nyingi. Pia, zinaweza kusaidia katika kuhifadhi uhai wa mimea na viumbe vinavyotegemea mimea hiyo.
Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Tanzania wanafanya juhudi za kuendeleza na kuhifadhi mbegu hizi, ikiwemo kuanzisha vituo vya kuhifadhia mbegu na kutoa elimu kwa wakulima kuhusu umuhimu wa kutumia mbegu za asili.