Sampuli za viwatilifu 1005 kati ya Sampuli 1025 nchini Tanzania zimekidhi vigezo vya kutumika kwa wakulima baada ya Mamlaka ya Afya ya mimea na viwatilifu Tanzania Plant Health and pesticides authority(TPHPA) kufanya utafiti na kujiridhisha kuanzia mwaka 2022 hadi 2023.
Akizungumza katika Maadhimisho ya Mimea Duniani Kaimu Mkurugenzi wa TPHPA Dkt. Joseph Ndunguru ni sampuli Ishirini Kati ya Sampuli 1025 za Viwatilifu ambazo zilibainika kuto kukidhi Vigezo.
Profesa Iringaa Kweka ni msimamizi wa Viwatilifu kutoka TPHPA amesema katika kuhakikisha kuwa mazo kutoka Tanzania Yanakubalika nje ya Nchi mamlaka imekuwa ikitumia maabara yenye Ithibati ili kupima Ubaora na Usama wa Chakula.
Aidha amesema Ithibati ya Maabara inasaidia kuleta maendeleo ya Kilimo nchini Tanzania na Kukuza Kipato kwa Ngazi ya Kaya
Maadhimisho ya Siku ya Mimea Dunia Hufanyika May 12 ambapo kwa mwaka huu Kauli mbiu inasema Mimea Yenye Afya Isaidia Kuondoa Njaa, Kupunguza Umasikini, Kutunza Mazingira na Kukuza maendeleo ya Uchumi.
No comments:
Post a Comment