Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip
Mpango amewasilisha kwa Rais John Magufuli taarifa ya kamati aliyoiunda
kuchunguza umiliki wa kampuni ya simu Airtel na kueleza jinsi Serikali
ilivyoingizwa mkenge.
Taarifa hiyo imewasilishwa baada ya Rais Magufuli kutoa agizo la kufanyika hivyo Desemba 20 mwaka jana.
Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo, Dk
Mpango alisema Serikali imejiridhisha kuwa ubinafsishaji wa Shirika la
Simu Tanzania (TTCL) kwenda Celtel, baadaye kuhamishiwa Zain na sasa
Airtel ulifanyika kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu.
Kufuatia ukiukwaji huo Dk Mpango amesema
Serikali inayomiliki asilimia 40 ya hisa za kampuni ya Airtel imeamua
kufanya mazungumzo na kampuni ya Airtel inayomiliki asilimia 60 ya hisa
ili nchi iweze kupata haki yake.
No comments:
Post a Comment