Asasi isiyo kuwa ya Kiserikali ya (SEIDA) ambayo Imekuwa ikijihusisha na Uimarisha wa Masoko ya Ndani ya Mazao ya Maharage inatarajia kupunguza Uhaba wa upatikanaji wa Mbegu hizo kwa kuzalisha mbegu kwa njia ya Umwagiliaji.
Hayo yamesemwa na Afisa Mradi kutoka Asasi hiyo Wilberth Wanga katika Warsha ya mafunzo ya Siku moja ya jinsi ya kuongeza thamani katika zao la Maharage.
Aidha ameongeza kuwa wanajitahidi kama mradi kutoa mafunzo kwa upandaji wa maharage pasipo kutegemea mvua peke yake na kuwapatia mbegu kwa ajili ya kuanzia lengo likiwa ni kuzalisha mbegu kwa wingi.
Bitrice Msafiri ni Mkurugenzi wa Kampuni ya (Bivac) ambayo inayo Jihuhusisha na Utoaji Elimu Kuhusu jinsi ya Kuongeza Thamani katika zao la Maharage ametoa wito kwa serikali kuwa na idadi ya wakulima ili kufahamu uhitaji halisi wa mbegu kwa wakulima.
Pia kwa upande wake mmoja ya wakulima ambaye amewahi kunufaika na mradi huo wa uongezaji thamani katika Maharage amesema bado wanasubiri mbegu hizo ambazo zinatarajiwa kuzalishwa na shirika hilo ili kupunguza changamoto hiyo.
Asasi ya (SEIDA) inashirikiana na mfuko wa kuendeleza mifumo masoko (AMDT) katika kufanikisha Mradi wa Kuhamasisha soko la ndani la la zao la Maharage kwenye lishe ya chaku;la linalo lenga upatikaji wa lishe Linganifu.
Wataalamu wa kilimo wanasisitiza kuwa kuwa maharage ni zao muhimu nchini Tanzania na ni zao la pili kwa umuhimu baada ya mahindi hivyo linapaswakulimwa kwa muktadha wa kibiashara na sio kwaa ajili ya kukidhi mahitaji ya familia pekee kwa kuweka juhudi katika kusambaza aina mpya za Mbegu.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Wilbert Wanga
Huduma :Afisa Mradi
Mahali : Simanjiro | Manyara
Kampuni : SEIDA
Contact : +255 622 78 37 51
+255 765 36 11 51
No comments:
Post a Comment