KOCHA wa Manchester United Erik Ten Hag ametoa kauli nzito kuhusu hatima ya nahodha wa klabu hiyo muingereza Harry Maguire.
Ten Hag amesema licha ya kuwa Maguire ni Nahodha wake lakini hiyo pekee haimpi uhakika wa kuanza kila mchezo.
“Nalisema hili haimanishi unapokuwa Nahodha basi unakuwa na haki ya kucheza kila mchezo hasa pale unapokuwa na Varane katika kikosi chako.” amesema Ten Hag akimuongelea Maguire.
Aidha katika hatua nyingine Kocha huyo raia wa Uholanzi amemmwagia sifa beki wa zamani wa real Madrid ambaye kwa sasa yupo katika kikosi chake cha Manchester United Rafael Varane kwa kubainisha kuwa hadhi aliyonayo na mafanikio aliyoyapata yana mchango mkubwa sana ndani ya kikosi hicho.
“Hadhi yake, mafanikio yake na yote aliyoshinda inaonesha kuwa anaweza kuwa na mchango mkubwa sana ndani ya kikosi chetu. Kwa upande wa timu kuna ushindani mkubwa na kuna michezo mingi na tunaweza kuona kila baada ya mchezo kujua ni nini hasa tunahitaji.”
Manchester United imekusanya jumla ya alama tatu katika michezo yake mitatu ya mwanzo ya Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kufunga klabu ya Liverpool kwa jumla ya mabao 2-1, huku ikiwa imetoka kupoteza michezo yake miwili dhidi ya Brighton and Hove Albion pamoja na Brentford
MAGUIRE AKALIA KUTI KAVU MANCHESTER UNITED
Utoaji wa tuzo umefanyika Oktoba 21 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere uliopo Posta, Dar es salaam.Tuzo hizo ziligawanyika katika makundi makuu matatu ambayo ni ligi kuu, Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), maarufu kama FA na Ligi ya Wanawake.
Kikosi bora cha Ligi ya Wanaume
1. Aishi Manula
2. Shomari Kapombe
3. Mohamed Hussein
4. Joash Onyango
5. Dickson Job
6. Mukoko Tonombe
7. Clatous Chama
8. Feisal Salum
9 . John Bocco
10. Prince Dube
11. Luis Miquissone.
Kikosi bora cha Ligi ya Wanawake;
1. Janeth Shija
2. Julieth Singano
3. Happy Hezron
4. Vaileth Nicholas
5. Fatuma Issa
6. Amina Bilali
7. Stumai Abdallah
8. Opa Clement
9. Aisha Masaka
10. Mawete Mussolo
KIKOSI BORA CHA LIGI KUU YA WANAWAKE NA WANAUME MSIMU 2020 / 2021
UWEZO mkubwa ambao amekuwa akiuonyesha kiungo mshambuliaji mpya wa Simba Msenegali, Pape Ousmane Sakho umewaibua makocha wa timu hiyo ambao wameweka wazi wanajivunia usajili wa nyota huyo, huku kocha Mkuu Didier Gomes akikitabiria makubwa kikosi hicho.
Sakho ameanza vizuri majukumu yake ndani ya Simba, ambapo juzi Jumamosi kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa maandalizi ya msimu dhidi ya FAR Rabat, aliifungia Simba bao moja kwenye mchezo ulioisha kwa sare ya mabao 2-2, huku akiwa nyota wa mchezo.
Nyota huyo alijiunga rasmi na Simba, Agosti 14, mwaka huu akitokea klabu ya Teungueth ya kwao Senegal, ambapo amekuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kilichoweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya kabla ya msimu ‘pre season’.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa kwanza kwake, aliwashangaza wengi kutokana na jinsi ambavyo alikuwa akiuchukua mpira na kuwafuata mabeki bila hofu.
Inaelezwa kuwa chenga zake za maudhi mara kwa mara ziliwalaza wapinzani chini ambapo alifanikiwa kuwaangusha wachezaji wa Rabbat mara mbili kutokana na chenga za maudhi.
Bao lake lilitajwa kuwa bora sana ambapo hadi kocha wa zamani wa Simba, Sven Vandebroeck alijikuta akishangilia kutokana na ubora wake.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Kocha wa viungo wa Simba, Adel Zrane alisema: “Nimekuwa na nafasi ya kuwafuatilia wachezaji wote ili kuhakikisha wanakuwa na utimamu tosha wa mwili, hivyo namfahamu Sakho vizuri ni miongoni mwa vijana wenye vipaji vikubwa ambao kama ataendelea kucheza katika kiwango hiki basi tutarajie makubwa.”
Naye kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes akizungumzia kikosi chake mara baada ya mchezo wa Jumamosi alisema: “Tumepata nafasi nzuri ya kujipima ni wazi tunapaswa kuendelea kuimarika zaidi ya hapa, naamini kikosi hiki kinaweza kufanya vizuri zaidi kuliko kile cha msimu uliopita.
“Tunapaswa kuwa wavumilivu, katika kipindi cha maandalizi tulichonacho na nina uhakika tutakuwa tofauti kabisa.”
SAKHO WA SIMBA MTU NA NUSU
Serikali kupitia wizara ya Michezo Imetakiwa kuupa Kipaumbele Mchezo wa Riadha kwa Watoto kuanzia Umri wa Miaka 6 hadi 14 ili Kuongeza Idadi ya Wanariadha nchini Tanzania.
Akizungumza Katika Kongamano lililowakutanisha wadau wa Michezo kutoka Taasisi Mbalimbali chini ya TAYAC Mkoani Arusha Katika Ukumbi wa Corridor Spring Hotel Suleiman Nyambui Mwanariadha wa zamani kutoka Tanzania amesema Vipaji vya Riadha haviibuliwa kwa watoto ukilinganisha na Zamani.
Nyambui Amesema ni aibu kwa taifa la Tanzania ambalo lina Wanariadha wengi kuishia kupeleka wanariadha watatu (3) katika Michezo ya Olympic nchini Japan licha ya Kuwa Uwezo wa Kupeleka zaidi ya wanariadha hao kwa Taifa kama Tanzania Upo.
Akitaja sababu kubwa ambayo Imefanya Tanzania kushuka Kiwango katika Riadha Duniani ukilinganisha na Mataifa mengine kama Kenya ni Kushindwa Kuwekeza kwa Watoto wakiwa bado wadogo ikiwa ni pamoja na kuibua Vipaji vya Ridha na Kuviendeleza.
Juliana Mwamsuva ni Mkurugenzi wa TAYAC Mkoani Arusha Yaani (Youth Athletics Championship) Taasisi isiyo ya Kiserikali ambayo ina nia ya Kuibua, Kujenga na Kuendeleza Riadha kwa Watoto kwa Kushirikiana na Wadau mbalimbali ili kuimarisha Riadha Tanzania.
Mkakati ambao TAYAC Imepanga kuufanya ni kuwa na wanariadha katika kila shule ya Msingi na Sekondari Mkaoni Arusha na Kuwafuatilia kwa Kutumia Mitandao na Kufuata Moja kwa moja.
Pia amesema watakuwa na Mshindano ambayo yatakuwa yaki wajumuisha Wanafunzi hawa ili kuendeleza kukuza Mchezo wa Riadha Mkoani Arusha na Tanzania kwa Ujumla na Michezo Mingine Ikiwemo kurusha Mkuki.
Hata hivyo amebainisha kuwa Lengo kuu la Kongamano ni wadau kutambua Fursa zilizopo katika Riadha na Kuwekeza ili Kukuza na Kurudisha Mchezo wa Riadha nchini Tanzania.
CHANZO CHA HABARI
Jina : TAYAC
Mahali : Mkoani Arusha
Contact : +255754 623517
TAYAC YAJA NA MIKAKATI YA KUINUA RIADHA UPYA NCHINI TANZANIA
Bonanza la Mpira wa Miguu lenye lengo la Kupima afya lililokuwa linafanyika Namanga Mkoani Arusha limehitimishwa kwa Namnga Worriors FC Kuibuka Mabingwa Mbele ya Maasai Worriors na kukabidhiwa Kombe lao.
Bonanza hilo lililo
fadhiliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Vuka Initiative lililopo Mkoani
Arusha lenye Lengo la kuhamasisha Vijana kupima afya, Kujitambua na Kuchukua
hatua wanapo Bainika na Maambukizi ya Magonjwa Mbalimbali.
Akikabidhi Kombe Hilo Mgeni
rasmi wa Mashindano hayo amewataka Vijana
kukumbuka kupima afya ikiwa ni njia ya Kujiweka Salama katika Maisha ya
Kila siku.
Vero Ignatus ni Mkurugenzi wa Vuka Initiative Mkoani Arusha
ambapo amesema Bonanza lilianza Tarehe Sita Mwezi wa sita Kata ya Longido
wilaya ya Longido Mkoani Arusha yenye Kauli Mbiu ya “Jali afya yako Pima Kwa
Hiari” ikiwa na lengo la kuwa kumbusha Vijana na Jamii kwa Ujumla Kupima afya
zao Kwa Hiari.
“Niwaase Vijana Wenzangu Usiogope Kupima afya yako unapo pima
afya yako na kujigundua kuwa una
maambukizi ina kuwa ni Rahisi wewe Kuanza Matibabu Mapema sio kwa maambukizi ya
Ukimwi tu na Hata Magonjwa Mengine” Alisema Vero Ignatus Mkuruenzi wa Vuka
Initiative.
Ignus Lwena Katibu wa
Chama cha Mpira wa Miguu Wila ya Longido Amewashukuru Vuka Initiative na
kampuni ya Kichina Inayojenga Mzani wa Kimokoa kwaletea Bonanza hilo na
kuhamasisha vijana Kupima afya ili kutatua changamoto ya Muda Mrefu ya
Vijana wa Wilaya hiyo Kuto kuwa na Mazoea ya Kupima Afya zao.
Hata hivyo kwa Upande wa
Kapteni wa Timu ya Maasai Worriors ambao walikuwa washindi wa Pili katika
Mchezo huo Baada ya Kufungwa na Namanga Worriors Wamesem a Licha ya Kuwa
Wamefungwa na Kuchukuwa Kombe katika Bonanza Hilo wakapime ili kujua Afya Zao.
Vuka Initiave ni Shirika
lisilo la Kiserikali ambalo limekuwa likijihusisha na Kupinga Ukatili na
Kuhamasisha vijana kujikinga na Magonjwa mbalimbali ikiwemo ya Kuambukiza na Yasiyo ya Kuambukiza.
Jina : Vuka Initiative
Mahali : Arusha
Contact : +255714903131