Wanandoa nchini wameaswa kupata mafunzo ya mara kwa mara ili kuzidi kuimarisha mahusiano yao kutokana na mabadiliko ya kitabia kunako chagizwa na Kukuwa kwa Utandawazi ambao unabadilisha mwenendo na kuwa sehemu Hatari.
Akizungumza baada ya Kongamano la Usiku wa wanandoa wapendanao lijulikanalo kama “BEST CHRISTIAN COUPLE’s AWARDS,” Askofu mkuu FPCT Tanzania, Bishop Stevie Mulenga amesema, “Makongamano kama haya ni ya muhimu sana hasa kwa wanandoa yanasaidia kukuonesha ni nini unatakiwa ufanye.
Bishop Stevie Mulenga pia ameeleza kuwa ndoa ni kama gari inavyohitaji kufanyiwa service baada ya muda husika.
“kwahiyo ndoa pia ni muhimu sana kuwa na vipindi kama hivi wanandoa mnakutana mnajengana.” Amesema Bishop Stevie Mulenga.
“Wanandoa mnapokuwa wawili sasa wewe na mke wako kila mtu anajipima ni wapi amepungukiwa ili afanye vizuri.” Bishop Stevie Mulenga.
Kwa upande wake Mke wa Katibu mkuu mstaafu FPCT, Anna Kuluzi, ameeleza kuwa wanandoa wanatakiwa kufuata utaratibu wa neno la Mungu ka alisemavyo.
Baadhi ya washiriki katika Tukio hili la “BEST CHRISTIAN COUPLE’s AWARDS,”
“Sisi tulifuate neon la Mungu linasema nini kuhusu masuala ya ndoa, sawa hali iko hivyo na dunia ipo hivyo lakini sisi turudi kwenye msingi wa ndoa ni nini,” amesema Anna Kuluzi.
Vilevile amesema kuwa Vijana ambao wapo kwenye ndoa wafuate huo msingi kujitoa na kuwa na mahusiano mazuri na Mungu kwani itawasaidia kufaulu katika ndoa zao.
Naye Katibu mkuu mstaafu FPCT, Dkt Jackson Kaluzi, amesemampaka sasa ametimiza miaka 40 ya Ndoa baina yake na mke wake Anna Kaluzi.
“Tulipokuwa tunakaribia Miaka hii 40 tuliamua badala ya kufanya sherehe yetu ya ndoa kanisani kama wengine tuliamua tuwe na kitu kama hiki mtoko wa wanandoa.”
“Tuliamua kwamba tuwakaribishe wanandoa kwamba wawe na siku yao ya kutoka.” Ameeleza Dkt Jackson Kaluzi.
Hata hivyo ameeleza kuwa katika nyakati za sasa ambapo ndoa nyingi zinavunjika ni muhimu kwa wanandoakutenga siku za kutoka pamoja na kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa watu wenye uzoefu kwenye ndoa na kujifunza Zaidi neno la Mungu.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Bishop Stevie Mulenga
Huduma : Askofu Mkuu Fpct Tanzania
Mahali : Arusha
No comments:
Post a Comment