Muimbaji wa nyimbo za Kidunia Maua Sama amesema kati ya vitu
anavyotamani kwenye muziki kwa sasa ni kujiingiza katika Muziki wa
Injili ‘Gospo’.
Akiongea na moja ya chombo cha habari nchini Tanzaniana Maua amesema kuwa, japokuwa ni Muislam lakini amejikuta akitamani siku moja
kuimba Injili.
“Napenda sana nyimbo za inspiration, kuna wakati nafikiria najikuta
nikitamani kuimba hasa hizi za Gospo.
Hata hivyo Ipo siku nitaimba kwa sababu ni
kitu ninacho-kipenda na kukitamani kutoka moyoni,” alisema Maua.
No comments:
Post a Comment