Imeelezwa kuwa Tatizo la Baadhi ya wakristo kushindwa kufunguliwa huku Baadhi ya Wakristo Wakifunguliwa tena Kwa wakati ni kwa sababu ya Neema aliyo nayo Mtumishi anaye Omba.
Akizungumaza katika Kipindi cha Top Ten ya Habari Maalum fm kinacho Peperushwa Kila Juma Mosi saa 11 Jioni hadi saa Moja Usiku Mtume Elia Mrutu wa Kanisa la Nuru ya Mataifa amesema Mtumishi anaweza kuwa chanzo cha Kumfungua au Kuto Kumfungua Mtu mbali na Muombewaji Mwenyewe.
“Neema aliyo pewa Mtu hauwezi fananisha na Neema ya Mtu Mwingine namaanisha Nguvu nilizopewa na Mungu ni Tofauti na Nguvu za Mtumishi mwingine ndivyo ilivyo hata kwa Nguvu ya Kuwafungua Watu wengine” Mtume Elia Mrutu.
Mtume Elia Amesema neema alizo Toa Mungu kwa watumishi wake ndizo zinazo Weka Utofauti wa Kuwafungua watu katika Matatizo mbalimbali au kushindwa kuwafungua watu.
Akizungumzia Moja Ya shuhuda ambazo Mungu alifanya kwa Kumtumia amesema Mungu alisha wahi Mtumia Kumponya Mtu ambaye alikuwa kichaa na alikuwa amepalalaizi kwa Miaka Mitano.
“Ilikuwa Mkoani Arusha nilipo kutana na Mama huyu ambaye alikuwa na Tatizo kwa Miaka Mitano nilimuombea alikuwa amefungwa kamba mikononi na alikuwa anashindwa kutembea Nilivyo omba Mungu alimfungua na Nikapigiwa simu na Watoto wake Kunieleza kuwa hali ya Mama Yao imekuwa Nzuri Kabisa na Sasa ni Mshirika Mzuri ndani ya Kanisa” Alisema Mtume Elia Mrutu.
Elia Mrutu ni Mtume na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Nuru Ya Mataifa lililopo Mianzini Mkoani Arusha nchini Tanzania akiwa na Miaka kumi katika Huduma Tangu ameianzisha.
CHANZO CHA HABARI
No comments:
Post a Comment