Mshereheshaji wa matukio mbali mbali ya kikristo na muandaaji wa matukio ya Harusi Ablenty Sadock kutokea Tanzania amewatia vijana moyo kufanya kazi kwabidii ili kuweza kutimiza malengo yao walio jiwekea bila kukata tamaa.
Akizungumza na kipindi cha Gospel Climax Kupitia Youtube Channel ya Habari Maalum Tv ambacho huwa kinazungumza Watumishi mbalimbali ili kuweza kuwatia moyo vijana wengine nao waweze kufikia ndoto zao.
Ablenty sadock amesema kuwa ili kuweza kupata kazi nilazima uweze kujitoa kwa moyo wako wote kufanya kazi hata kama ni ndogo ili iweze kukufungulia milango ya kazi nyingine kutokana na ubora wakazi hio.
Aidha amesema kuwa kwasasa amefungua Ofisi yake ambayo itaweza kuwasaidia watu kumpata endapo watakua wanauhitaji kwenye sherehe zao watakua wanampata kwa urahisi kwenye ofisi yak.
‘’Mtu anaweza akaja ofsini nakutuachia shughuli yake kila kitu kitafanyika ,ishu ya mapishi, usafiri, keki, vile vile kwenye matukio ya harusi wale ambao wanahitaji ushauri au namna ya kuandaa sherehe kile nilichonacho naweza nikashirikiana nao”’ Amesema Sadock.
Hatahivo amewashauri vijana kutokata tamaa kwa vile vitu ambavyo wanapenda kuvifanya ili kuweza kutengeneza kesho yenye manufaa makubwa kwani mfano mzuri ni yeye mwenyewe hakuwahi kukata tamaa hadi kufika alipofikia sasa.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Ablenty Sadock
Huduma : Mwimbaji na Mshehereshaji
Mahali : Arusha
Contact : +255 652 86 19 61
No comments:
Post a Comment