Askofu wa kanisa la FPCT Tanzania Mch. Stevie Mulenga amewataka wafanyakazi wa Taasisi zinazosimamiwa na kanisa hilo kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuendelea kujenga mwili wa Yesu Kristo.

Askofu Mulenga ameyasema hayo katika ziara ya kutembelea taasisi za kanisa hilo zilizopo Jijini Arusha ambapo amepokelewa na viongozi na wafanyakazi ikiwemo Habari Maalum Media, Idara ya Maandiko Kimahama na Chuo cha Habari Maalum.

Akizungumzia  mafanikio na mipango ya kituo cha Habari Maalum Media Mkurugenzi Yusto Swai  ameshukuru kwa ujio wa Kiongozi huyo  na kuwatia moyo katika utendaji wao wa kazi  ambapo amesema kuwa wameweza kufikisha injili kwa watu wote kupitia vipindi vya redio na Tv.

Kwa upande wa wafanyakazi pamoja na viongozi wa taasisi hizo wamepokea maangizo ya askofu wao na kuahidi kufanya kazi kwa bidii kwa ushirikiano.

ASKOFU MULENGA : TAASISI ZIFANYE KAZI KWA USHIRIKIANO TUTAONA MATOKEO

No comments:

Post a Comment