Wahitimu wa mafunzo ya Theolojia Ngazi ya Astashahada Chuo cha Biblia Sanjaranda Tawi la Gongali na Meserani Arusha wametakiwa kutumia elimu waliyoipata kuleta mabadiliko chanya kwenye kanisa na jamii kwa ujumla.
Rai hiyo imetolewa na Askofu wa FPCT Jimbo la Arusha Mch. Ayoub Muna katika mahafali ya kwanza yaliyofanyika Mesereni Arusha ikijumuisha matawi mawili ya chuo cha Biblia Sanjaranda tawi la Gongali na Meserani ambapo jumla ya wahitimu 28 wamehitimu masomo ya theolojia kwa ngazi astashada.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Sanjaranda Elibariki Steven Chima amewapongeza wahitimu hao kwa hatua hiyo na amewataka kujiendeleza zaidi badala ya kuishia kwenye ngazi ya astashahada na kujifunza kwa vitendo yale waliyoyajifunza.
Nao baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wameahidi kutumia vyema elimu waliyopata kwa Kumtumikia Mungu na kuleta mabadiliko kwenye kanisa na jamii kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment