MCHUNGAJI MSUYA : MSHINDI ANA MOYO WA KUSHINDA HATA KABLA YA KUSHINDA

 

Na Method Charles


Mchungaji Kiongozi wa Kanisala EAGT Mirerani Frank Msuya   amehimiza wakristo kuamini katika  Ushindi katika somo aliliofundisha  kwenye Ibada ya Jumapili.

 Akizungumza  Katika kipindi cha Gospel Climax  kinacho peperushwa  kupitia Youtube Chanel ya Habari Maalum Media  Mch Frank Msuya amesema amefundisha somo hilo kwa sababu mshindi ni yule mtu ambaye ana moyo wa kushinda kabla haja shinda hivyo aamini ya kwamba yeye ni mshindi.

 Mchungaji Msuya amesema  mtu ambaye anamuamini Kristo Yesu  Yeye ni mshindi pia ametoa mfano wa mtu moja ambaye alikuwa anaitwa Samsoni kuwa alikuwa ni mshindi Kwasababu walimtoboa macho lakini Samsoni alikuwa bado ni mshindi kwakuwa alikuwa anania ya ushindi ndani yake.

 Aidha naye Rehema Joseph Mshirika katika kanisa hilo  amesema amejifunza kuwa yeye ni mshindi pia anawashauri watu wawe washindi kwasababu watashinda wakimwamini kristo ndani yao na wakiokoka.

Hata hivyo   Tomas Edward Moja ya washirika katika Kanisa hilo amewataka  watu kuamini katika ushindi na wajifunze kumtegemea Mungu kwa kila jambo na watashinda Mambo yote.

 Kanisa la EAGT Mererani Mkoani Manyara ni moja ya kanisa ambalo limekuwa likihudumia Wakristo zaidi ya 100 kiroho na kuwaongoza njia ya Kwenda Mbinguni chini ya Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo Mchungaji Frank Msuya.

 

Chanzo cha Habari

KANISA : EAGT MERERANI

UJUMBE : MSHINDI

CONTACT : +255763990033

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment