Wakristo wametakiwa kumuabu Mungu katika Roho na Kweli Badala ya kuamini katika dini kuwa ni Mpango wa Mungu katika Kumuabudu.
Akihubiri katika Ibada ya Jumapili Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Naivera Church Apostolic Tanzania Lililopo Arusha Bishop Dkt Julius Laizer amesema Kumuabudu Mungu kuna anza na Mtu ambaye Ameokoka.
Amesema Mkristo hawezi kumuabudu Mungu katika Roho na Kweli kama hajaokoka kwani Yesu ndiye amepewa Mamlaka na Mungu ya Kutawala Dunia na Vitu vyote Vilivyopo ndani Yake.
Aidha amebainisha kuwa kuokoka sio Dini Mpya Kuokoka ni kuzaliwa mara ya Pili kwani kuzaliwa mara ya kwanza ni kile kipindi ambacho mwanadamu anazaliwa kutoka Tumboni mwa Mama yake.
Hata hivyo Sanjari na Hilo Bishop Laizer ameeleza kuwa Wokovo ni Malango wa kumfungulia Mtu njia ya Kuanza Kumuabudu katika Roho na Kweli.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Bishop Dkt.Julius Laizer
Huduma : Naivera Church Apostolic
Mahali : Arusha
Mamlaka : NCA
Contact : +255 74436865
No comments:
Post a Comment