Na Joyce Daniel
Mwimbaji wa nyimbo za injili Elisante Nnko Amewaomba wadau wa muziki kushiriki katika Tamasha kubwa la Muziki wa Injili ambalo lina lengo la kuzindua nyimbo tatu zinazo patikana katika mfumo wa Video.
Akizungumza na Method Charles katika kipindi cha Top Ten kinachopeperushwa na Habari Maalum fm iliyopo mkoani Arusha nchini Tanzania amesema tamasha hilo kila Mmoja anaweza Kushiriki kwani Hakuna Kiingilio.
Amesema kuwa Tamasha hilo litafanyika tarh 9/10/2022 Maeneo ya USA river katika kanisa la leganga FPCT Miembeni kwa Askofu Boniface Nnko.
Aidha amesema kuwa kutakuwa na waimbaji mbalimbali ikiwemo Yusto Onesmo,Anna Annie, Rebecca Magaba,Dani Safari,Agness mayagila, Esther yunus,Papai shengoma,na waimbaji wengi watakuwepo.
Elisante Nnko ni mwimbaji na Mtayarishaji wa Muziki wa Injili Nnchini Tanzania lakini pia amekuwa akijihusisha na Huduma ya Maombi na Maombezi kupitia Facebook Page Elisante Nnko na Amefanyika msaada kwa Wengi.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Elisante Nnko
Huduma : Mwimbaji wa Nyimbo za Injili
Mahali : Arusha
Contact : +255 752613240
No comments:
Post a Comment