Tamasha hilo lililopewa jina la "international tour Experience" litafanyika katika nchi mbalimbali huku akiweka wazi kuwa amejiandaa vizuri na ugonjwa wa uviko 19 kwake sio kikwazo.

Akizungumza Kuhusu hilo, Joel Lwaga amesema kwa Mwaka huu imekua neema kwake kutokana na Kuanza rasmi tamasha lake la kuzunguka nchi mbalimbali kwa lengo la kutoa Burudani na kuona kwa namna gani Muziki wa Injili unafika mbali zaidi.

"Nitaanza nchini Ghana ,Nigeria,Kenya ,Uganda na nchi zingine nyingi lengo ni kuutangaza Muziki wetu wa injili ambapo tamasha Hilo litamalizika mwakani mwezi agosti."

Hata hivyo, amesema ametaja Siri inayofanya Mashabiki zake kuupenda Mziki wake hususani rika mbalimbali. “Mashairi yangu ni vitu ambavyo vinanigusa binafsi hivyo navoona watu wanapenda kazi zangu ni wazi kuwa ujumbe Umefika kwa haraka zaidi kutokana na kuguswa kwao na kuguswa mioyo yao kutokana na tungo zangu".

Pia Lwaga amewaahidi Mashabiki zake kuwa hivi karibuni ataachia wimbo mpya aliomshirikisha Msanii kutoka nchi za nje .

"Tour yangu itajumuisha na kufanya video kwa ajili ya baadhi ya kazi zangu ambazo audio tayari nimeshafanya hivyo nnategemea tour hii nitafanya vitu mbalimbali ikiwemo kolabo na Wasanii mbalimbali ambao tayari nimeshazungumza nao."

JOEL LWAGA RASMI ZIARA KIMATAIFA "INTERNATIONAL TOUR EXPERIANCE"

No comments:

Post a Comment