Serikali kupitia wizara ya Michezo Imetakiwa kuupa Kipaumbele Mchezo wa Riadha kwa Watoto kuanzia Umri wa Miaka 6 hadi 14 ili Kuongeza Idadi ya Wanariadha nchini Tanzania.

Akizungumza Katika Kongamano lililowakutanisha wadau wa Michezo kutoka Taasisi Mbalimbali chini ya TAYAC Mkoani Arusha Katika Ukumbi wa Corridor Spring Hotel Suleiman Nyambui Mwanariadha wa zamani kutoka Tanzania amesema Vipaji vya Riadha haviibuliwa kwa watoto ukilinganisha na Zamani.

Nyambui Amesema ni aibu kwa taifa la Tanzania ambalo lina Wanariadha wengi kuishia kupeleka wanariadha watatu (3) katika Michezo ya Olympic nchini Japan licha ya Kuwa Uwezo wa Kupeleka zaidi ya wanariadha hao kwa Taifa kama Tanzania Upo.

Akitaja sababu kubwa ambayo Imefanya Tanzania kushuka Kiwango katika Riadha Duniani ukilinganisha na Mataifa mengine kama Kenya ni Kushindwa Kuwekeza kwa Watoto wakiwa bado wadogo ikiwa ni pamoja na kuibua Vipaji vya Ridha na Kuviendeleza.

Juliana Mwamsuva ni Mkurugenzi wa TAYAC Mkoani Arusha Yaani  (Youth Athletics Championship) Taasisi isiyo ya Kiserikali ambayo ina nia ya Kuibua, Kujenga na Kuendeleza Riadha kwa Watoto kwa Kushirikiana na Wadau mbalimbali ili kuimarisha Riadha Tanzania.

Mkakati ambao TAYAC  Imepanga kuufanya  ni kuwa na wanariadha katika kila shule ya Msingi na Sekondari  Mkaoni Arusha na Kuwafuatilia  kwa Kutumia Mitandao na Kufuata Moja kwa moja.

Pia amesema watakuwa na Mshindano ambayo yatakuwa yaki wajumuisha Wanafunzi hawa ili kuendeleza kukuza Mchezo wa Riadha Mkoani Arusha na Tanzania kwa Ujumla na Michezo Mingine Ikiwemo kurusha Mkuki.

Hata hivyo amebainisha kuwa Lengo kuu la Kongamano ni wadau kutambua Fursa zilizopo katika Riadha na Kuwekeza ili Kukuza na Kurudisha Mchezo wa Riadha nchini Tanzania.

CHANZO CHA HABARI

Jina : TAYAC

Mahali  : Mkoani Arusha

Contact : +255754 623517

TAYAC YAJA NA MIKAKATI YA KUINUA RIADHA UPYA NCHINI TANZANIA

No comments:

Post a Comment