Moshi. 

 Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Martin Shao na Mbunge wa Moshi mjini, Priscus Tarimo wamejitokeza kuchanjwa chanjo dhidi ya virusi vya corona,  huku wakiwataka wananchi kuepuka upotoshaji wa mitandaoni.

Shughuli ya kuchanja chanjo ya hiyo imeanza asubuhi leo Jumanne Agosti 3, 2021 katika hospitali ya rufaa ya KCMC huku makundi ya watu wenye umri mkubwa na watumishi wa Afya wakiwa ni miongoni mwa waliojitokeza.

Akizungumza mara baada ya kuchanja, Askofu mstaafu Shao aliyeambatana na mkewe, aliisihi jamii kutafuta taarifa kutoka vyanzo sahihi kuhusu usalama wa chanjo kwa kuwa katika mitandao ya kijamii, kuna baadhi ya taarifa potofu.

“Nimekuja hapa leo kuchanja kwa sababu natambua umuhimu wa chanjo na tunashukuru serikali kwa kufanya mchakato huu lakini KCMC nao wameweka utaratibu mzuri sana. Shughuli inafanyika kwa weledi na haraka,” amesema.

"Tuache kuwatia hofu watanzania na serikali ifanye kila inalowezekana kujibu upotoshaji wowote huo ili sasa suala la kuchanja liwe ni la hiyari ya mtu. Narudia tena tusitiane hofu. Wataalamu wametuhakikishia chanjo ni salama,"

Hata hivyo Mbunge wa Moshi mjini, Priscus Tarimo amesema ameamua kuchanja ili kujikinga yeye mwenyewe na maambukizi ya corona lakini pia aweze kuwalinda familia na wananchi wengine na kutaka jamii kupuuza propaganda mbaya dhidi ya chanjo.

ASKOFU AONYA KUHUSU UPOTOSHAJI JUU YA CHANJO

No comments:

Post a Comment