Moshi. 

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo amesema kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kutaka kukutana na viongozi wa vyama vya siasa nchini itatibu majeraha mengi na kudumisha umoja na mshikamano.

 Alhamisi Aprili 22, 2021 wakati akilihutubia Bunge, kiongozi mkuu huyo wa nchi amesema atakutana na viongozi wa vyama vya siasa kuweka mwelekeo wa kuendesha shughuli za siasa zenye tija na maslahi kwa nchi.

Amesema amedhamiria kuendelea kulinda misingi ya demokrasia, uhuru wa watu na vyombo vya habari na kubainisha kuwa uhuru na demokrasia ni msingi wa amani katika nchi na husaidia kuchochea maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Akichambua hotuba ya Samia, mkuu huyo wa KKKT amesema kauli zake zinaendelea kuleta matumaini kwa Watanzania na kuonyesha uwezo walionao wanawake.

"Mama ametoa hotuba nzuri iliyotoa mwelekeo mzuri kwa Taifa, imewatia watu matumaini na hili la kukutana na viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani ni jambo jema sana, ninampongeza kwa hilo na ninaamini itakuwa sehemu ya kuponyesha majeraha waliyokuwa nayo wanasiasa,” amesema.

Kuhusu suala la haki kwa mahakama amesema "Hili ni jambo ambalo limekera Watanzania wengi, kwa mahakama kushindwa kutenda wajibu wake, sasa inapaswa kusimamia haki na kuona haki inatendeka."

ASKOFU SHOO : RAIS SAMIA ATATIBU MAJERAHA KWA WANASIASA

No comments:

Post a Comment