Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo [TEMDO] kwa kushirikiana na bodi ya sukari nchini imekuja na mkakati wa kutatua tatizo la sukari kwa kuanzisha viwanda vidogovidogo.
Meneja wa Utafiti na Ubunifu Mhandisi Patrick Kivanda amesema kuwa tayari wapo kwenye mkakati wa kuanzisha kiwanda chenye uwezo wa kutengeneza tani ishirini za sukari kwa siku ili kupunguza uhaba wa sukari nchini.
Amesema Viwanda hivyo wataweza kugawa katika mikoa mbalimbali ambayo imekuwa i ikizalisha miwa kwa wingi ili kuounguza upatikanaji wa sukari nchini.
Hata Hivyo ameongeza kuwa kwa sasa wapo kwenye mpango wa kutekeleza kwa vitendo utengeneza wa viwanda hivyo ambapo vitakuwa msaada wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment