Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imetoa mafunzo ya njia bora za uzalishaji wa mbegu za maharageya lishe ili kupunguza uhaba wa mbegu nchini Tanzania.
Akizungumza kuhusu mafunzo hayo mkurugenzi wa BIVAC Company Limited ambao ni waratibu wa mafunzo hayo Bitrice Msafiri amesema wametoa mafunzu hayo kwa Maafisa kilimo Thelathini (30) na wakulima watano watakao wasimamia wakulima kufuata kanuni bora za kilimo.
Yusuph Kisuzi ni makaguzi wa mbegu kutoka taasisi ya Kudhibiti Ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) ambaye pia ni Muwezeshaji wa Mafunzo hayo amesema kuna uhaba wa mbegu za maharage ya asili nchini Tanzania ukilinganisha na Mbegu za chotara.
Mgeni Rasmi Katika ufunguzi wa Mafunzo hayo Yaliyo fanyika taasisi ya Uhandisi na usanifu wa Mitambo (TEMDO) Mkurugenzi Profesa Fredrick Kahimba amesema mafunzo haya yatasaidia wakulima kulima maharage lishe Kulimwa kwa ubora ambao unasabaisha vile virutubisho vinaendelea kuwepo kuanzia shambani hadi vinapo mfikia mlaji.
Baadhi ya wanufaika wa Mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yatasaidia kuongeza upatikanaji bora wa mbegu za maharage lishe na kuimarisha Soko la maharage lishe nchini Tanzania.
Inaelezwa kuwa Maharage na kunde
ni mazao makuu ya jamii ya mikunde yaliyozalishwa Tanzania kwa mwaka wa kilimo
2022/2023 huku ikielezwa kuwa jumla ya
hekta laki 892,786 zilipandwa maharage na kunde, ambapo wakulima wadogo
walipanda eneo la hekta 889,557 na mashamba makubwa yalipandwa hekta 3,229.
No comments:
Post a Comment