Klabu ya Liverpool itatakiwa kutoa kitita cha paundi milioni 52.75 ili kukamilisha usajili wa kiungo Naby Keita kutoka klabu ya RB Leipzig.

Liverpool walifikia makubaliano ya kumsajili kiungo huyo katika dirisha la usajili wakati wa majira ya joto mwaka 2017 huku dau la usajili likitegemea klabu ya RB leipzig ingemaliza nafasi ya ngapi katika msimamo wa ligi ya Ujerumani ‘Bundesliga’.

Kama Leipzig wangepata nafasi ya kushiriki katika michuano ya klabu bingwa, ingewalazimu Liverpool kutoa paundi milioni 59 kumpata kiungo huyo lakini sasa watatoa paundi milioni 52.75 kutokana na klabu hiyo kumaliza msimu ikiwa nafasi ya sita.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amekuwa akimuwinda kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 ili kuimarisha kikosi chake katika safu ya kiungo na sasa Keita atakuwa mchezaji rasmi wa Liverpool ifikapo tarehe 1 mwezi July mwaka huu.

  Keita ameichezea RB Leipzig jumla ya michezo 39 katika msimu wake wa mwisho akifunga mabao 9 na kutoa pasi saba za magoli.

Keita kutua Anfield kwa dau hili

No comments:

Post a Comment