PADRI ROGER : SHULE ZINAZZO TOA HUDUAMA KWA JAMII ZIPATE MSAMAHA WA KODI

 





KILIMANJARO

SERIKALI imeombwa kuweka mazingira rahisi kwa shule binafsi za sekondari hasa za kidini nchini zinazotoa huduma kwa jamii kupata msamaha wa kodi badala ya mfumo uliopo sasa kuonekana wote ni wafanyabiashara.

Mfumo wa sasa wa kuomba vibali vya msamaha wa kodi umekuwa na changamoto na maelezo mengi huku ukitofautiana baina ya mkoa mmoja na mwingine.

Mkuu wa shule ya Maua seminari inayomilikiwa na Kanisa Katoliki nchini, iliyopo Mkoani Kilimanjaro, Padri Roger Massawe amesema hayo na baada ya serikali kutoa tamko la kutaka shule za sekondari binafsi ziombe leseni ya kufanya biashara. 

Hata hivyo mwanasheria mkuu wa serikali Profesa Adelardus Kilangi amekiri kupokea changamoto kama hiyo katika shule nyingine nchini kuhusu mfumo wa uendeshaji wa taasisi binafsi za elimu nchini na kuziomba taasisi hizo kuwa na ustahimilivu kwani atalifikisha katika mamlaka husika ili liweze kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu. 



No comments:

Post a Comment