Na Method Charles
Askofu mkuu wa kanisa la KKKT Kanda ya Kaskazini Askofu Saimoni Masangwa amefanikiwa kuzindua Wodi mpya na ya Kisasa Katika Hospital a Serian NNgaramtoni ambayo itasaidia kupunguza Tatizo la vyumba ya Kulaza Wagonjwa katika Hospital hiyo.
Akizindua Wodi hiyo ambayo itachukua wagonjwa Zaidi ya 200 ambao watakuwa wakilazwa amesema wamekuwa na mpango wa Muda mrefu wa kuboresha wodi zote zilizopo katika Hospital ya Serian Ngaramtoni na Huu ni Mwanzo tu wataendelea kuboresha wodi zote ili ziwe katika mfumo wa kisasa.
Askofu Masangwa amesema mbali na wafadhili ambao wamewakuwa wakijitoa amewataka wale wote wenye mapenzi mema na Hospital ya Serian Ngaramtoni kuendelea kuchangia ili kuweza kuboresha huduma za afya zinazo tolewa katika hospital hiyo ili kuwa katika viwango vya Kimataifa.
Daktari Amon Marti ni Mkurugenzi katika Hospital ya Serian Ngara mtoni ambayo ipo chini ya Kanisa la KKKT Tanzania amesema hospital hiyo ilikuwa na vitanda 160 na kwa sasa Wodi hiyo mpya ina itanda 54 jumla kwa sasa hospital hiyo itakuwa na vitanda 214 katika wodi zote.
Daktari Amon amesema kuwa Changamoto kubwa ambayo walikuwa wanaipata hapo awali kabla ya Woodi hiyo kujengwa ilikuwa ni Uchakavu wa Wodi na kwa ukarabati wa wodi hii ya kisasa wananchi watafurahi kuhudumiwa katika Mazingira Mazuri.
Fransisca Kivuyo ni Muuguzi Mkuu wa Hospital ya Serian Ngaramtoni amesema wamekuwa wakihudumia wagonjwa wa mkundi mbalimbali wakiwemo Masikini na Matajiri kulingana na Kipato cha Mtu na pia wanapokea BIMA zote za afya.
Wodi mpya ya Kisasa iliyo zinduliwa inauwezo wa kuchukua wagonjwa 54 huku katika Chumba kimoja wakilazwa wagonjwa watatu, vyumba Binafsi akilazwa mtu mmoja huku kila chumba kikiwa na choo na Bafu Maaalum la kisasa lenye Maji Moto na Baridi huku pia kukiwa na Mfumo Maalum wa Kuwasiliana na Muuguzi Mgonjwa anapo kuwa na uhitaji wowote.
Chanzo cha Habari
Mkurugenzi Selian Ngaramtoni :Dkt. Amon Israel Marti
Contact : +255754744232
Mahali : Arusha Ngaramtoni.
No comments:
Post a Comment