Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Tanzania Fina Akyo amesema Tamasha la Uzinduzi wa Albamu yake Mpya ya UMWEMA litakuwa na utafauti mkubwa tofauti na ilivyo zoeleka katika Matamasha Mengine.
Fina ameyasema hayo Wakati akizungumza na Method Charles katika kipindi cha Gospel Climax kinacho Tazamwa kupitia Youtube Channel ya Habari Maalum Tv.
Amesema angeweza kufanya uzinduzi huo Mapema kabla ya mwezi wa tisa ila kwasababu ya tatizo la ugonjwa wa korona ilipelekea kukatisha swala la Uzinduzi huo.
Fina kyoo anaye fanya Vizuri na Wimbo wake wa Umwema anatarajia kuzindua album yake aliyo itambulisha kwa Jina la Umwema Jumapili ijayo ya September 13, 2020 katika kanisa la mlima Sinai lililopo Arusha kisongo Ghorofani kwa mchungaji Zakaria Malima
Tamsha hili la Uzinduzi litaanza Mapema Baada ya watu kutoka kanisani Majira ya saa saba mchana na Kuendelea.
Aidha amewaomba Watu Arusha kufika katika Tamasha hilo la Uzinduzi wa Albamu ya Umwema ambalo litashehene waimbaji mbalimbali kutoka Arusha ambao wamekuwa wakitamba na Nyimbo mbalimbali kama Vile Janet Kahembe, Daniel Isingo, Vaileth Daniel na Wengine wengi.
Hata hivyo Fina amesema katika uzinduzi huo Mungu ataonyesha utofauti wake hasa vile atakavyo jitukuza kupitia nyimbo zake na utukufu wa Mungu kutawala
No comments:
Post a Comment