Wakristo wametakiwa kufahamu kuwa ipo tofauti kati ya uzima wa milele na
uzima wa ulimwengu kwani watu wengi hufikiri maisha waliyonayo hayana
mwisho na ndiyo mitazamo ya watu wengi.
Akihubiri
kwenye ibada ya jumapili katika kanisa la KKKT Dayosisi ya Meru Jimbo
la Magharibi Usharika wa Patandi Mch.Gwarisa Mwaipopo kutoka katika
Dayosisi ya Mashariki na Pwani amewataka wakristo kutambua kuwa wapo
katika ulimwengu usio dumu.
Hata hivyo amehitimisha kwa kuwataka wakristo kufahamu kuwa palipo na uzima kuna baraka na neema na palipo na mauti kuna laana na mabaya.
No comments:
Post a Comment