Mchungaji, Moses Emena na kiongozi wa taasisi ya Mibosco ameiomba
serikali kusaidia watoto wa kike ambao wanaishi katika mazingira magumu.
Ameyasema hayo Kunduchi jijini Dar es salaam wakati wa mahafali ya
wahitimu wa ufundi Cherehani waliosaidiwa kusomeshwa na taasisi hiyo.
Aidha, ameoiomba serikali na wadau mbalimbali kusaidia watoto wa kike ambao wamekuwa wakiishi katika maisha magumu.
“Serikali na jamii kwa ujumla ninaiomba kuwasaidia hawa watoto,
kumsadidia mtoto wa kike ni kumuwezesha kuweza kujikwamua katika maisha
yake,”amesema Mchungaji Emena
No comments:
Post a Comment