SERIKALI
ya Mkoa wa Tabora imewaagiza Maofisa Ugani kuhakikisha watoa elimu kwa
wakulima kulima mazao yote kitaaalamu na kwa kuzingatia kanuni za kilimo
bora ili kuwaongezea uzalishaji wa mazao mbalimbali na tija.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wilayani
Igunga baada ya kujionea mazao mbalimbali yakiwemo mahindi na choroko
zikiwa zimepandwa bila kuzingatia vipimo vinavyotakiwa kitaalamu.
Alisema
kuwa kanuni za kilimo bora haziwezi kuwa kwa ajili ya mazao ya biashara
ya tumbaku na pamba pekee bali ni lazima sisitizwe kutumika katika kwa
mazao yote yanalomwa mkoani humo ili uzalishaji uongezeke na
Halmashauri ziwe kupata kodi zaidi.
Mwanri
kuwa kitendo cha Maofisa Ugani kuwaacha wakulima kuendelea kulima kama
walivyozoea bila kuzingatia kanuni za kilimo bora kinaoonyesha kuwa
watumishi hao hawajatimiza majukumu yao vema.
Alisema
kuwa kazi kubwa ya Maofisa Ugani ni kumsaidia mkulima ili haweze
kuondokana na kilimo duni na hatimaye alime kisasa kwa ajili ya
maendeleo yake na Taifa kwa ujumla.
Mwanri
alisema kuwa wakulima wamekuwa wakijutumia kulima maeneo makubwa lakini
mavuno hayalingani na nguvu walizotumia kwa sababu ya kukosa ushauri wa
kitaalamu wa kuwahimiza ujazaji wa mazao katika shamba na matumizi ya
mbolea.
Alisema
kuwa kuanzia mwakani hatamuonea huruma Afisa Ugani yoyote ambaye kwenye
eneo lake la kazi atakuta mkulima amelima bila kuzingatia nkanuni za
kilimo bora badala yake amepanda ovyo ovyo katika shamba lake.
Naye
Mshauri wa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Modest Kaijage alisema
kuwa suala la upandaji kwa kuzingatia vipimo ni kwa ajili ya mazao yote
na kuongeza ni vema Maofisa Ugani wote kuanzia ngazi ya vijiji hadi
Wilaya kuhakikisha wanahimiza wakulima kuzingatia vipimo ili waweze
kupata mazao mengi.
Alisema
kuwa wakati muda wa kupanda alizeti umekaribia ni vema Maofisa Ugani
wote wakaanza kuhimiza wakulima walime zao hilo kwa vipimo vinavyotakiwa
.
Kaijage
alisema kuwa hatua hiyo itawasaidia wakulima kulima eneo dogo lakini
ambalo litakuwa na mimea mingi iliyopandwa katika umbali unaotakiwa
kitaalamu ambalo litampa mkulima mavuno mazuri
No comments:
Post a Comment