Katika Kuadhimisha siku ya Hedhi Salama Serikali Imetakiwa kujenga na kutenga Vyumba maalumu katika shule za Msingi na Sekondari kwaajili ya Kumsaidia Mtoto wa Kike kubadili Taulo anapo kuwa katika wakati wa hedhi pindi anapo kuwa shule ili kuepuka adha ya Kupitwa na Vipindi vya Masomo Darasani.
Hayo Yamesemwa na Msimamizi wa elimu ya Uzazi na Malezi Shuleni na Mitaani Kutoka Maternity Africa Christine Jastine wakati akikabidhi Taulo za Kike katika Kuadhimisha siku Hedhi Duniani May 28 katika shule ya Msingi Lesinoni iliyopo wilayani Arumeriu Mkoani Arusha.
John Kilusu ni Mkuu wa Shule ya Sekondary Lesinoni ambapo amesema wanamshuku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasani kwa kuwaongezea Vyuma vya madarasa na Mashimo ya Vyoo ambayo yalijumuisha Chumba maaalum Kwaajili ya Matumizi ya wanafunzi wa Kike pindi wanapo kuwa Hedhi.
Aidha Kwa Upande wake Mwalimu wa Malezi kutoka Shule hiyo Jackline Sevele ameipongeza Maternity Africa kwa elimu ya uzazi na hedhi salama ambayo wamekuwa wakiitoa katika shule hiyo kwani inawasaidia kujitambua na kuondokana na Dhana Potofu.
Licha ya Serikali Kufungua Milango kwa watoto wa kike kupata Elimu bado Watoto wa kike walio Shuleni nchini Tanzania wanakabiliwa na Changamoto ya Upatikanaji wa taulo za Kike Pedi kujistili wanakuwa katika Siku zao hasa katika maeneo ya Vijijini.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Kivulini Maternity Africa
Huduma : Kutoa Taulo za Kike
Mahali : Arusha
Mamlaka : Kivulini Maternity Africa
Contact : +255 717468185
No comments:
Post a Comment