Arusha
Shirika lisilo la Kiserikali linajihusisha na afya kwa kijana na jamaii zuia madhara yatokanayo na Pombe na Madawa ya Kulevya Blue Cross Society Tanzania Limezindua kampeni iitwayo najivunia kuto kutumia Madawa ya kulevya ili kuwasaidia vijana katika shule za msingi na sekondari wasijiingize Katika matumizi ya madawa ya kulevya.
Akizungumza mara baada ya Kuzindua kampeni Hiyo Afisa mradi kutoka Blue Cross Tanzania Anna Panga katika shule ya msingi na Sekondari Ngarenaro mkoani arusha amesema kwa kutumia Kampeni vijana wamekuwa wakielewa Zaidi elimu ya afya kwa kijana na jamaii zuia madhara yatokanayo na Pombe na Madawa ya Kulevya.
Eva Mringi ni makamu mkuu wa shule ya msingi Ngarenaro ambaye amebaini kuwa kampeni nah ii itawasaidia wanafunzi kujitambua na kuto kujiingiza katika matuizi ya madawa ya kulevya na badala yake kujikita katika masomo na kuongeza ufaulu.
Moja ya Muhanga wa Madawa ya kulevya ambaye alitumia madawa ya kulevya kwa miaka Zaidi ya Ishirini na Baadae Kuacha amewaasa viijana kuacha kuacha tabia ya kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya kwani inavuruga hatima ya maisha.
Nao baadhi ya Wanafunzi kutoka shule ya msingi Ngarenaro wamesema kampeni hiyo inaendelea kuwakumbusha na kuwasidia kujikita Zaidi katika masomo.
Tanzania ipo nafasi ya tano kwa idadi ya watumiaji wa bangi barani Afrika, inaongoza eneo la Afrika mashariki ikiwa na watu milioni 3.6 wanaotumia bangi ikifuatiwa na Kenya ambayo iko nafasi ya sita na watu milioni 3.3 na Uganda katika nafasi ya nane ikiwa na watumizi milioni 2.6.
No comments:
Post a Comment