Idara ya Maendeleao ya Mtoto Jiji la Arusha kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Blue Cross Tanzania zimewakutanisha viongozi wa madawati ya kupinga ukatili ndani na nje ya shule kutoka shule mbalimbali jijini Arusha ili kuwajengea uwezo katikakupambana na Ukatili.
Akizungumza mara baada ya semina hiyo Afisa Maendeleo jiji la Arusha Habiba Madebe amebainisha kuwa kuwakutanisha wajumbe wa kumlinda mtoto nje na ndani ya Shule ni muendelezo wa harakati za kupambana na ukatili na kuimarisha madawati shuleni.
Revocatus Nginila ni Mkurugenzi mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali Blue Cross Tanzania ambapo amesema katika kupambana na ukatili eneo la shule wamekakabidhi Boksi za kutoa Taarifa zinazo husiana na Ukatili katika shule mbalimbali zilizopo katika Jiji hilo.
Moja ya washiriki katika semina hiyo ya kuwajengea uwezo Samweli Gunda ameeleza kuwa mafunzo haya yatasaidia kupungungza vitendo vya ukatili ndani nan je ya Shule.
Kwa Mujibu wa Ofisi ya Katibu mkuu wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia wanawake na makundi Maalum Inaeeleza kuwa ukatili dhidi ya watoto katika mazingira ya Ndani na nje ya shule ni moja wapo ya sababu inayo changia baaadhi ya watoto kuacha shule na kujihusisha na shughuli Hatarishi ambazo hazina faida kwa mtoto.
No comments:
Post a Comment