Imeelezwa kuwa moja ya sababu inayochangia Mtoto kujiingiza katika Matumizi ya Madawa ya kulevya ni kukosekana kwa ukaribu kati ya mzazi na Mtoto.
Akizungumza mara Baada ya Kumaliza mafunzo ya njia Bora kwa kijana na jamaii juu ya kuzuia madhara yatokanayo na Pombe na Madawa ya Kulevya Iliyofanyika Katika Shule ya Msingini Sinoni Mkoani Arusha afisa mradi kutoka Blue Cross Society Tanzania Gloria Vicent amesema ukaribu wa mtoto na Mzazi ni njia ya kumuepusha mtoto na Matumizi ya Madawa ya Kulevya.
Akibainisha sababu zinazo changia Kuwepo kwa ongezeko la wanafunzi ambao wamekuwa wakitumia madawa ya Kulevya katika Baadhi ya shule Muhanga wa Madawa ya Kulevya amesema ni Marafiki na makundi ya wanafunzi ambao hawana madili katika Jamiina wapo mbali na wazazi wao.
Grase Mbwambo ni moja ya Mwanafunzi kati ya shule ya msingi Sinoni Mkoni Arusha Ambapo amesema Mafunzo hayo ya Kupambana na Madawa ya Kulevya yatasaidia kuongeza ufaulu kwa mwanafunzi mmoja mmoja kwani itawafanya wanafunzi kuto jiingiza katika Madawa ya Kulevya na badala yake kujikita katika Masomo.
Kwa Mujibu wa Ripoti kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kupambana na dawa za kulevya na uhalifu, UNODC Barani Afrika, asilimia 70 ya watu wanaopata matibabu dhidi ya dawa za kulevya wako chini ya umri wa miaka 35.
No comments:
Post a Comment