Arusha
Watafiti wametakiwa kutoa suluhisho katika Tafiti Mbalimbli ambazo wakekuwa wakizifanya ili kuwasaidia wakulima kupambana na Magonjwa na kuzalisha mbegu bora za Mharage na Mahindi.
Hayo yamesemwa na Mtafiti kutoka Taasisi ya Tafiti za Mbegu Tanzania Tari Selian Arusha Richard Temba wakati wa mafunzo ya uzalishaji Mbegu za maharage lishe kwa vijana Zaidi ya hamsini kutoka mkoani Manyara semina iliyo fanyika Mkoani Arusha katika ofisi za Taasisi hiyo.
Bitrice Msafiri ni Mratibu wa Mfunzo kutoka Bivac Tanzania ambao wamekuwa wakijihushi na utoaji elimu kwa vijana kuhusu Maharage Lishe amesema wameamu kufikia vijana Zaidi ya hamsini kutoka wilaya za Mkoani wa manyara ili kuwabadilisha na kuwashawishi wakulima kulima maharage kilimo Biashara.
Baadhi ya wakulima walioshiriki katika mafunzo hayo Kutoka mkoani Manyara wamesema awali walikuwa wanalima maharage pasipo kuzingatia mbegu gani zilikuwa zinahitajika katika soko baada ya Mfunzo wataanza kuzalisha mbegu hizo ili kujiingizia kipato.
Wakulima walioshiriki mafunzo hayo ni kutoka mkoani Manyara katika Wilaya za Babati, Hanang na Wilaya ya Simanjiro.
Tafiti zinaeleza kuwa wazalishji wa mbegu za maharage lishe nchini Tanzani ni wacache ukilinganisha na wazalishaji wa mahindi na nafaka zingine hali ambayo inahitajika jitihada za kutosha kutia uzalishaji wa mbegu hizo
CHANZO CHA HABARI
Jina : Bivac Company Limited
Huduma : Mafunzo
Mahali : Arusha
Mamlaka : Bivac Company Limited
Contact : +255 621 59 18 71
No comments:
Post a Comment