Katika Kupambana na ukatili shuleni Zaidi ya Kamati Nane za Ulinzi na Usalama kwa mtoto ndani na Nje ya Shule mkoni Arusha zimejengewa uwezo ikiwa ni Muendelezo wa kumarisha madawati ya kupinga ukatili ndani na nje ya shule kutoka shule mbalimbali jijini Humo.
Akizungumza nje ya Semina ya kuwa jengea uwezo wajumbe wa kumlinda mtoto nje na ndani ya Shule Afisa elimu kutoka Blue Cross Tanzania Gloria Vicent amesema lengo la kuwajengea uwezo kamati hizi za ulinzi wa mtoto ni kupunguza matukio ya ukatili nje na ndani ya Shule.
Eva Mringi ni Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngarenaro amesema vitendo vya Ukatili katika maeneo ya Nyumbani na Shuleni Vitambungua kwani Semina hiyo imewawezesha njia sahihi ya kuripoti matukio na Matukio na aina ya Matukio yanayo takiwa kuripotiwa.
Baadhi ya wanafunzi ambao ni wajumbe katika kamati za ulinzi na Usalama wa Mtoto ndani ndani na nje ya Shule wamesema watawashikisha wanafunzi wenzao kuhusu njia salama ya kuripoti matukio ya ukatili ikiwemo kutumia Maboksi ya Maoni na kushiriki katikakupambana na ukatili.
Kwa Mujibu wa Ofisi ya Katibu mkuu wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia wanawake na makundi Maalum Inaeeleza kuwa ukatili dhidi ya watoto katika mazingira ya Ndani na nje ya shule ni moja wapo ya sababu inayo changia baaadhi ya watoto kuacha shule na kujihusisha na shughuli Hatarishi ambazo hazina faida kwa mtoto.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Blue Cross Tanzania
Huduma : Semina
Mahali : Arusha
Mamlaka : Blue Cross Tanzania
Contact : +255 758 89 13 45
No comments:
Post a Comment