Licha ya uwepo wa soko kubwa la zao la korosho nje ya nchi, baadhi ya wadau wa zao la korosho wameiomba serikali kuangalia upya utaratibu wa upatikanaji wa vibali na tozo kwani ni kikwazo kwa wadau hao katika kuyafikia masoko hayo.
Hayo yamebainishwa kwenye kikao cha mwaka cha wadau wakilimo na jukwaa huru la wadau wa kilimo kilicholenga kujadili fursa mbalimbali ikiwemo fursa za masoko ambayo imeonekana kuwa changamoto kwa wakulima wengi wakiwemo wa zao la korosho.
Akifunga mafunzo hayo mkurugenzi mtendaji wa ANSAF , Honest Mseri amesema wamebaini kuwa ili wakulima waweze kuzalisha kwa tija na kuuza bidhaa zao nje ya nchi nguvu kubwa inatakiwa kutumika kuimarisha vyama vya akiba na mikopo kwa wakulima , wafugaji na uvuvi.
No comments:
Post a Comment