Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 21 wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wamemchagua Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. Alex Malasusa kuwa Mkuu wa KKKT mpya mteule akichukua nafasi ya Askofu Dkt. Fredrick Shoo aliyemaliza muda wake wa uongozi wa awamu mbili.
Askofu Malasusa anarejea tena kwenye nafasi hiyo aliyoihudumu kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2015 alipomaliza na kuikabidhi kwa Askofu Shoo.
Mwenyekiti wa Uchaguzi huo uliofanyika Jijini Arusha, Askofu Amon Mwenda, amesema kura zilizopigwa zilikuwa 241 ambapo kati ya hizo Malasusa amepata kura 167 sawa na asilimia 69.3 huku Askofu Abednego Kesho Mshahara akipata kura 73 sawa na asilimia 30.3.
No comments:
Post a Comment