Mkazi wa Mtaa wa 14 Kambarage Mjini Geita, Martine John anadaiwa kujiua kwa kujinyonga baada ya kudaiwa kumjeruhi mkewe, Justina Paulo (34) kwa kitu chenye ncha kali kwa kile kinachodaiwa wivu wa mapenzi.

 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Adam Maro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ingawa amesema hawezi kulizungumzia zaidi kwa kuwa yupo safarini.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita, Mfaume Salum akizungumza na waandishi wa habari leo, Novemba 23, 2023 amesema wamempokea mwanamke huyo ambaye amelazwa hospitalini hapo baada ya kukatwa sehemu ya koromeo, kichwani na mkononi na kitu chenye ncha kali.

“Novemba 22 saa tano asubuhi tulipokea mwanamke katika idara yetu ya dharura akiwa na majeraha kwenye shingo, mkono na kichwani. Majeraha haya yanaonyesha yamekatwa na kitu chenye ncha kali. Eneo la shingo jeraha ni kubwa, amekatwa sehemu ya koromeo na anaendelea na matibabu,” amesema Dk Salum.

Mama mzazi wa mwanamke aliyejeruhiwa, Anastazia Paulo akizungumzia maisha ya wanandoa hao, amesema wamekuwa na mgogoro wa mara kwa mara uliosababisha mwanae kurudi nyumbani, japo imeelezwa siku za karibuni mume wake alimfuata baada ya kusuluhishwa na kurudi kuendelea na maisha.

AJINYONGA BAADA YA KUDAIWA KUMJERUHI MKEWE NA KITU CHENYE NCHA KALI

No comments:

Post a Comment