Baraza la Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste (CPCT) mkoa wa Arusha linatarajia kuongeza idadi ya makanisa ambayo hayajasajiliwa na Baraza hilo  kwa kufanya makongamano katika wilaya mbalimbali nchini Tanzania ili kuwafikia wachungaji waliopo wilayani hasa Vijijini.

Hayo Yamesemwa na Askofu wa Fpct Jimbo la Arusha na Mwenyekiti Mpya wa Cpct Arusha mchungaji Ayoub Munna katika Ibada ya kusimikwa kwa viongozi wa umoja wa makanisa ya kipentekoste (CPCT) mkoa wa Arusha amabayo imefanyika July 20,2023 ambapo viongozi kutoka makanisa mbalimbali wamehudhuria tukio hilo.

Mchungaji Munna amekula kiapo cha kutumika katika nafasi ya mwenyekiti wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Jiji la Arusha (CPCT) baada ya aliyekuwa kiongozi wa Muda huo Askofu Oral Sossy kumaliza Muda wake ambapo amesema atakuwa mstari wa mbele kusimamia maono yote ya Baraza la umoja huo.

Katibu mkuu mteule wa umoja wa makanisa ya kipentekoste (CPCT) mkoani Arusha Dkt. David Mollel ambaye pia ni Askofu wa (TAG) Jimbo la Arusha Kati amesema ni wakati sahihi kwa makanisa ya kipentekoste kuungana na kushirikiana kupinga vitendo viovu bila kubaguana ili kulinda taswira ya Baraza la umoja huo.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika tukio hilo ambaye amemuwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha Bishop Dkt. Israel Ole Maasa amesema mkuu wa mkoa anaheshimu umoja wa makanisa yote ya Kikristo ambapo ameahidi kuwapa ushirikiano pale wakati wowote kwa kuwa makanisa yana mchango mkubwa katika jamii.

Viongozi walio Simikwa ni Mwenyekiti Mchungaji Ayoub Munna wa Kanisa la Fpct Kimahama ambaye pia ni Askofu wa FPCT Jimbo la Arusha ambapo awali Mwenyekiti alikuwa Askofu wa (TAG) Jimbo la Arusha Bishop Oral Sossy.

Makamo Mwenyekiti aliyesimikwa ni Bishop Shadrack Kin'gori wa Kanisa la EAGT 

Katibu mpya wa Baraza la Umoja wa makanisa ya Kipentekoste (CPCT) ni Dkt. David Mollel ambaye pia ni Askofu wa (TAG) Jimbo la Arusha Kati.

Wajumbe wa Baraza la CPCT Mkoa ni Bishop Dkt. Israel Maasa wa kanisa la Pentecoste International  na Sadick Kinaga wa Kanisa la  Maranatha  Christian  Centre.

Baraza la CPCT mkoa  huundwa na Wawakilishi Watano akiwemo Mwenyekiti Makamo Mwenyeki, Katibu na Wajumbe wawili.

Wengine walio Simikwa ni Viongozi wote wa Baraza ngazi ya wilaya  katika wilaya zote saba za mkoa wa Arusha.

Mgeni wa Heshima alikuwa Mwenyekiti wa CPCT  Taifa Bishop Dkt. Barnabas Mtokambali aliye wakilishwa na Makamo Mwenyekiti wa CPCT Taifa Bishop Dkt. Daniel Awete.

Inaelezwa kuwa Ibada hiyo ya kusimikwa kwa viongozi wa Baraza la makanisa ya Kipentekoste mkoa wa Arusha (CPCT) imehudhuriwa na watumishi kutoka makanisa mbalimbali mkoani Arusha Ikiwemo baadhi yao kutoka (TEC), (CCT) huku lengo likiwa ni  kulinda amani na kueneza ukristo kwa kutumia Baraza la umoja.

 CHANZO CHA HABARI

Jina : CPCT Mkoa wa Arusha

Huduma :Uinjilishaji

Mahali  : Arusha

Mamlaka : Huduma Ya Injili

Contact : +255 767 05 75 28

VIONGOZI WAPYA WA BARAZA LA UMOJA WAMAKANISA (CPCT) WASIMIKWA MKOANI ARUSHA

No comments:

Post a Comment