MERERANI : Kiongozi wa kanisa la Efatha Mtume
na Nabii Josephat Elias Mwingira
anatarajia kutoa kiasi cha shilingi Milioni 10 kwaajili ya kurekebisha uwanja
wa (CCM) Mererani sehemu zilizo haribika baada ya Uwanja kufurika Kupita Kiasi.
Mtume na Nabii Mwingira alitamka
hayo siku ya nne na ya mwisho katika Mkutano mkubwa wa injili ambao Umefanyika Mererani
Mkoani Manyara.
“Nimeambiwa huu uwanja ni wa (CCM) Merarani nitachangia kiasi cha shilingi
milioni 10 kwaajili ya ukarabati wa uwanja huu” Alisema Mtume na Nabii Josephat
Mwingira wa Kanisa la Efatha Ministry.
Amesema Hayo Kufutia Kuharibika
kwa uwanja huo katika Baadhi ya maeneo yaa uwanja huo baada ya kufurika watu kupita kiasi ambao walitoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha,
Manyara na Kilimanjaro kuhudhuria mkutano wa injili.
Inaelezwa kuwa uwanja wa (CCM) Mererani ulikuwa mdogo ukilinganishwa na umati wa watu waliofika katika Mkutano huo Mkubwa wa Injili ambao ulianza July 26 na Kutamatika July 29, 2023.
Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira kutoka Kanisa la Efatha Ataendelea na ratiba ya Mkutano wa Injili akiizunguka Tanzania nzima huku mkoa wa Kilimanjaro ukifuata August 02 hadi August 05, 2023.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira
Huduma : Mkutano wa Injili Efatha Ministry
Mahali : Mererani
Mamlaka : Huduma Ya Injili
Contact : +255 622 60 00 00
No comments:
Post a Comment