Wito umetolewa kwa jamii kuwa na utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara kwa kuwa kuna baadhi ya magonjwa ambayo dalili zake hazionekani kwa haraka.
Rai hiyo imetolewa na Daktari
bingwa wa magonjwa ya ndani kutoka Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center
Dkt.Wailesy Adam kufuatia kufanyika kwa kambi ya uchunguzi na ushauri bure ambayo
imefanyika hospitalini hapo ikilenga magonjwa yasiyoambukiza ikiwa ni mwendelezo wa kuadhimisha Miaka 50 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kasikazini Kati .
Vilevile ameeleza kuwa mwitikio wa watu kujitokeza kupata matibabu hayo pamoja na ushauri ni mzuri ambapo lengo lao la kufanya kambi hiyo ni kupunguza idadi ya waathirika wa magonjwa yasiyoambukiza.
Afisa lishe wa Hospitali hiyo Bi. Salma Ally Muhammed ameitaka jamii kubadili mtindo wa maisha kwa kuzingatia lishe bora pamoja na kufanya mazoezi ili kuepuka kupata magonjwa yasiyoambukiza.
Nao baadhi ya Wananchi waliojitokeza kupima afya zao wamesema ni muhimu kuwa na utaratibu wa kuchangamkia fursa za matibabu bure ambazo zinatolewa na vituo mbalimbali vya afya ili kujua hali ya afya zao.
Hospitali hiyo imefanya uchunguzi wa matibabu pamoja na kutoa ushauri kwa jamii juu ya magojwa yasiyoambukiza kwa muda wa siku mbili ambayo yamehitimishwa June 2 huku kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO Ikielezwa kuwa magonjwa yasiyo ya Kuambukiza yanaongoza kwa vifo Duniani.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Dkt.Wailesy Adam
Huduma :Daktari
Mahali : Arusha | Ngaramtoni
Kampuni : Arusha Lutheran Medical Center
Contact : +255 692 053 707
No comments:
Post a Comment