Wanafunzi wa shule ya sekondari Losikito iliyopo mkoani Arusha wamepewa elimu ya afya ya uzazi na namna ya kujikinga na magonjwa yatokanayo na afya ya uzazi.
Mkufunzi kutoka taasisi ya Maternity Africa Arusha Einoti Godwin ameeleza lengo la kutoa elimu ya afya ya uzazi mashuleni hasa kwa vijana ni kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali kipindi cha mabadiliko ya ukuaji.
Chanzo cha Habari kilifanikiwa kumfikia mwalimu wa nidhamu na malezi katika shule hiyo Mwl Daudi Yunda ameishukuru taasisi ya mantenite Africa kwa kuweza kuwafikia vijana wao na kuwapa elimu ambayo itawasaidia kujitambua na kupunguza matukio ya ujauzito shuleni hapo.
Nao baadhi ya wanafunzi shuleni hapo waliopatiwa elimu hiyo wamezungumzia walichojifunza na kueleza umuhimu wa elimu hiyo ambayo inawajenga na kuwabadilisha kimtazamo.
Tafiti zinaeleza kuwa afya ya uzazi ni suala ambalo ni muhimu katika jamii yoyote, lakini upatikanaji wa huduma hiyo hukabiliwa na changamoto mbalimbali na hivyo kuwaweka wasichana na wanawake katika mazingira magumu.
No comments:
Post a Comment