Wito umetolewa kwa Mama Mjawazito kuwahi Kliniki mara baada ya kujigundua kuwa anapresha ya Mimba ili kupata maelekezo ya kitaalamu ya namna ya kujiepusha na matatizo yatokanayo na ujauzito.
Akizungumza Mwandishi wa Habari katika Kipindi Cha Morning Shine ya Habari Maalum Fm Dr Braiton Nyumayo kutoka Hospitali ya Kivulini Maternity Africa Iliyopo Ngaramtoni ya Chini Arusha amesema Mama mjawazito anawajibu kuhudhuria Kliniki wiki tatu kabla ya tarehe za makadirio ya kujifungua ili kujiepusha na madhara yatokanayo na mimba ikiwemoa presha na kifafa cha Mimba.
Aidha Dr Braiton amewashauri wakina mama wanaotaka kubeba ujauzito kuwa na utayari na Kuhudhuria Kliniki ili kujiepusha na dalili za hatari zinazoweza kupoteza maisha ya mtoto.
Nao baadhi ya akina mama wamesema madhara yanayowapata hasa pale wanapochelewa kuhudhuria Kliniki ni kupoteza maisha ya mtoto pamoja na mama kupata magonjwa ambayo yana athiri mfumo wa uzazi.
Hivi karibuni serikali kupitia wizara ya afya ilisema kiwango cha vifo vya watoto wachanga kabla ya kutimiza mwezi mmoja vimepungua kutoka vifo 37 kwa mwaka 1990 na kufikia vifo 18 kwa mwaka 2021.
No comments:
Post a Comment