Shirika la Kimataifa la Vijana Gospel Foundation Internationa Limezinduliwa rasmi Mkoani Arusha kwa lengo la kuwanganisha Vijana wenye Vipaji kutoka mataifa Mbalimbali Duniani ili waweze kunafaika na kukuza Uchumi kupitia Viapaji walivyo navyo.
Akizungumza katika Uzinduzi wa shirika Hilo ulio fanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Habari Maalum Mkoani Arusha Mkurugenzi wa shirika hilo Elisha Kazimoto amesema shirika Hilo lina washirika kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Kazimoto amesema Dhumuni la Kuanzishwa kwa Shirika hilo ni Kuimarisha Uchumi kwa kwa Vijana ili waweze kunufaika Kupitia Vipaji walivyo navyo wakiwa ndani ya Yesu kufuatia Jamii kushindwa kuliamini Kundi la Vijana.
Aidha Kwa Upande wake Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa shirika hilo ambaye Pia ni Mkuu wa Chuo cha Habari Maalum Nestory Ihano amesema Vijana wa Kikristu ni wakati wao kuona Fursa na Kuzitumia.
Dkt Timothy John ni mratibu wa shirika hilo ambaye amebainisha kuhusu shirika litakavyo kuwa likitekeleza shughuli zake na kuwafikia vijana huku akitaja mataifa amabayo tayari ni washirika wake kuwa ni Hispania,India, Pakstani, Kenya na Zimbabwe huku akibainisha kuwa watatumia vijana walio na Vipaji kutoka Kanisani.
Moja ya Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Sua mkoani Morogoro Joan Sikawa ambaye amejiunga na shirika hilo amebainisha kuwa kupitia shirika hilo anaamini kuwa atatimiza Ndoto zake.
Inaelezwa kuwa Kipaji Kinapo tumika kwa usahihi kwa kijana humsaidia kijana kujiingizia Kipato na kugeuza kuwa chanzo kitega uchumi na ajira ya Kudumu katika maisha ya Kila siku.
No comments:
Post a Comment