Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un amepiga marufuku mikusanyiko
inayoashiria kusherehekea sikukuu ya Krismasi kama vile inayohusu
unywaji na uimbaji.
Ametaka wananchi kutosherehekea sikukuu hiyo na wanaopenda kufanya
hivyo, waitumie Desemba 24 kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa bibi yake
aliyezaliwa siku kama hiyo mwaka 1919.
Kiongozi huyo ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha
vinadhibiti mikusanyiko yote ambayo inaendana na maadhimisho ya
Krismasi.
“Ni marufuku watu kukusanyika na kufanya mambo kama ya unywaji au kuimba katika sikukuu ya Krismasi,” chanzo kimoja cha habari kimenukuu taarifa ya kiongozi huyo.
Kim Jong Un amekuwa akichukua hatua kuzuia kuenea kwa utamaduni wa
kigeni na amedhibiti vyombo vya habari kutotangaza taarifa zozote
zinazoienzi sikukuu hiyo kama hatua ya kupiga marufuku Krismasi.
Ingawa sikukuu ya Krismasi si tukio kubwa nchini humo, lakini baadhi
ya wananchi wamekuwa wakiisherekea na kufuata misingi ya Kikristo.
No comments:
Post a Comment