amii ya Watu wenye Ulemavu Imetakiwa Kumuhubiri Mungu kwa Vitendo Badala ya Kubweteka na Kuamini hawawezi kumtumikia Mungu kwa Sababu ya aina ya Mapungufu waliyo nayo.
Akizungumza katika kipindi cha Top Ten ya Habari Maalum fm wakati akitambulisha Nyimbo zake Mwalimu na Mwimbaji wa nyimbo za Injili ambaye ni Mlemavu wa Viungo Mageuzi Kamkeni amesema ulemavu wa Viungo Isiwe Chanzo cha Kushindwa Kumtumikia Mungu.
Kamkeni Amebainisha kuwa Walemavu wamekuwa wakijitenga na Kazi za Mungu katika Kuhubiri Injili kwa Kujiona Hawawezi licha ya Kuwa kila Mtu Mungu ameweka Kipawa Chake ndani Yake Kwaajili ya Kumtumikia.
Aidha Mwalimu Mageuzi Kuhusu Nyimbo Amesema Nyimbo zake alizo zitambulisha ni Hawahi wala Hachelewi na Hakuna Lisilo wezekana ambazo Zinapatika katika katika Platfom Mbalimbali Ikiwemo Spotify, Youtube, Audio Mark pamoja na Apple.
“Tatizo la wakristo wali wengi wanasikiliza Nyimbo katika mlengo wa Kuburudika na sio Kupokea Majibu kupitia Nyimbo hizo hali hii wasitegemee kuwa wanaweza kutumia Nyimbo na Mungu akawajibu kuna Nyimbo za Kuburudika Ndio na Kuna nyimbo ambazo zikitumika zinaweza Badilisha maisha ya watu” alisema Mwalimu Mageuzi Kamkeni.
Mwalimu Mageuzi amebainisha Kuwa yupo Tayari Kufanya Kazi katika sehemu Yoyote atakayo kuwa amealikwa kwaajili ya Kumtumikia Mungu.
Kitaalumu Mageuzi Kamkeni licha ya Kuwa ni Mlemavu ni Mwimbaji wa Nyimbo za injili pia ni Mwalimu wa Masomo ya Sayansi kati shule ya sekondari Oldonyowasi.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Mageuzi Kamkeni
Huduma : Mwimbaji na Mwalimu
Mahali : Arusha | Oldonyosambu
Kanisa : Fpct ebenerzer Oldonyowasi
Contact : +255 764 58 96 03
No comments:
Post a Comment