Katika Kuadhimisha siku ya Hedhi Salama Serikali Imetakiwa kujenga na kutenga  Vyumba maalumu katika shule za Msingi na Sekondari kwaajili ya Kumsaidia Mtoto wa Kike kubadili Taulo  anapo kuwa katika wakati wa hedhi  pindi anapo kuwa shule ili kuepuka adha ya Kupitwa na Vipindi vya Masomo Darasani.

 

Hayo Yamesemwa na Msimamizi wa elimu ya Uzazi na Malezi Shuleni na Mitaani Kutoka Maternity Africa Christine Jastine  wakati akikabidhi Taulo za Kike katika Kuadhimisha siku Hedhi Duniani May 28 katika shule ya Msingi Lesinoni iliyopo wilayani Arumeriu Mkoani Arusha.


John Kilusu ni Mkuu wa Shule  ya Sekondary Lesinoni ambapo amesema wanamshuku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasani kwa kuwaongezea Vyuma vya madarasa na Mashimo ya Vyoo ambayo yalijumuisha Chumba maaalum Kwaajili ya Matumizi ya wanafunzi wa Kike pindi wanapo kuwa Hedhi.


Aidha Kwa Upande wake  Mwalimu wa Malezi kutoka Shule hiyo  Jackline Sevele ameipongeza Maternity Africa  kwa elimu ya uzazi  na hedhi salama ambayo wamekuwa wakiitoa  katika shule hiyo kwani inawasaidia kujitambua na kuondokana na Dhana Potofu.


Licha ya Serikali Kufungua Milango kwa watoto wa kike kupata Elimu bado Watoto wa kike walio Shuleni  nchini Tanzania wanakabiliwa na Changamoto ya Upatikanaji wa taulo za Kike Pedi kujistili wanakuwa katika Siku zao hasa katika maeneo ya Vijijini.

 

 CHANZO CHA HABARI

Jina : Kivulini Maternity Africa

Huduma : Kutoa Taulo za Kike

Mahali  : Arusha

Mamlaka : Kivulini Maternity Africa

Contact : +255 717468185

 

MATERNITY AFRICA WATOA TAULO ZA KIKE SHULE YA SEKONDARI LESNONI WILAYA YA ARUSHA DC




Katika Kupambana na  ukatili shuleni Zaidi ya Kamati Nane  za Ulinzi na Usalama kwa mtoto ndani na Nje ya Shule  mkoni Arusha zimejengewa uwezo ikiwa ni Muendelezo wa kumarisha madawati ya kupinga ukatili ndani na nje ya shule kutoka shule mbalimbali jijini Humo.

 

Akizungumza nje ya Semina ya kuwa jengea uwezo wajumbe wa kumlinda mtoto  nje na ndani ya Shule  Afisa elimu kutoka Blue Cross Tanzania Gloria Vicent amesema  lengo la kuwajengea uwezo  kamati hizi za ulinzi wa mtoto  ni kupunguza matukio ya ukatili nje na ndani ya Shule.


Eva Mringi ni  Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngarenaro amesema  vitendo vya Ukatili katika maeneo ya Nyumbani na Shuleni Vitambungua kwani Semina hiyo imewawezesha njia sahihi ya kuripoti matukio na Matukio na aina ya Matukio yanayo takiwa kuripotiwa.


Baadhi ya wanafunzi ambao ni wajumbe katika kamati za ulinzi na Usalama wa Mtoto ndani ndani na nje ya Shule wamesema watawashikisha wanafunzi wenzao kuhusu njia salama ya kuripoti matukio ya ukatili ikiwemo kutumia Maboksi ya Maoni na kushiriki katikakupambana na ukatili.


Kwa Mujibu wa Ofisi ya Katibu mkuu wizara ya Maendeleo  ya Jamii Jinsia  wanawake na  makundi Maalum Inaeeleza kuwa ukatili dhidi ya  watoto katika mazingira  ya Ndani  na nje  ya shule  ni moja wapo  ya sababu  inayo changia  baaadhi ya watoto  kuacha shule  na kujihusisha na  shughuli Hatarishi ambazo hazina faida kwa mtoto.

 

 CHANZO CHA HABARI

Jina : Blue Cross Tanzania 

Huduma : Semina

Mahali  : Arusha

Mamlaka : Blue Cross Tanzania

Contact : +255 758 89 13 45

 

USALAMA NA ULINZI WA MTOTO WAIMARISHWA MKOANI ARUSHA : BLUE CROSS TANZANIA


 

Wananchi waliothirika na mafuriko Arumeru na Karatu wamepatiwa msaada na Kanisa la new life pryer center chini ya mchungaji Ezekiel Odero Mombasa nchini Kenya.

 

Kanisa hilo limetoa kiasi cha Tsh Milioni 50 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko.

 

Akizungumza mara baada ya kufika katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda Mchungaji Ezekiel Odero amesema kuwa Tanzania ni nyumbani hivyo kupitia huduma ya Mungu anayofanya ni vyema kuwajali wale ambao wamepatwa na majanga hayo.

PASTOR EZEKIEL ATOA MILIONI 50 KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MKOANI ARUSHA

 

 

 


Idara ya Maendeleao ya Mtoto Jiji la Arusha kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Blue Cross Tanzania zimewakutanisha viongozi wa madawati ya kupinga ukatili ndani na nje ya shule kutoka shule mbalimbali jijini Arusha ili kuwajengea uwezo katikakupambana na Ukatili.

 

Akizungumza mara baada ya semina hiyo Afisa Maendeleo jiji la Arusha Habiba Madebe  amebainisha kuwa  kuwakutanisha wajumbe wa kumlinda mtoto  nje na ndani ya Shule ni muendelezo wa harakati za kupambana na ukatili na kuimarisha madawati  shuleni.


Revocatus Nginila ni Mkurugenzi mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali Blue Cross Tanzania ambapo amesema katika kupambana na ukatili eneo la shule wamekakabidhi Boksi za kutoa Taarifa zinazo husiana na Ukatili  katika shule mbalimbali zilizopo katika Jiji hilo.


Moja ya washiriki katika semina hiyo ya kuwajengea uwezo Samweli Gunda ameeleza kuwa mafunzo haya yatasaidia kupungungza vitendo vya ukatili ndani nan je ya Shule.


Kwa Mujibu wa Ofisi ya Katibu mkuu wizara ya Maendeleo  ya Jamii Jinsia  wanawake na  makundi Maalum Inaeeleza kuwa ukatili dhidi ya  watoto katika mazingira  ya Ndani  na nje  ya shule  ni moja wapo  ya sababu  inayo changia  baaadhi ya watoto  kuacha shule  na kujihusisha na  shughuli Hatarishi ambazo hazina faida kwa mtoto.

BLUE CROSS TANZANIA WATOA MASANDUKU MASHULENI KUPAMBANA NA UKATILI MASHULENI