Mamlaka ya dawa na vifaa tiba Tanzania TMDA imewataka wananchi kutoa taarifa pindi wanapopata athari wakati wanapotumia dawa.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja TMDA Kanda ya kaskazini Dkt.Vivian Wonanji wakati akiwa katika viwanja vya nanenane kuwa ni muhimu kutoa taarifa wakati mtumiaji wa dawa anapobaini madhara ili hatua za uchunguzi zichukuliwe mapema.
Ameongeza kuwa hatua ambazo wanazichukua kwa dawa zinazoleta madhara au maudhi madogo ni pamoja na kufanya ufuatiliaji wa dawa husika.
Moja kati ya wauzaji wa duka la Dawa za Binadamu Ngaramtoni amesema ili utumie dawa kwa usahihi ni muhimu kupima ili ujue tatizo na kupata huduma sahihi.
Ameshauri pia kwa watumiaji wa dawa ambao wamepata madhara kuwa ni vyema kutoa taarifa mapema ili kupata msaada wa haraka.
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ina jukumu la kulinda afya ya jamii kwa kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa dawa, chanjo, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na udhibiti wa bidhaa za tumbaku.
Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2022, TMDA imefanikiwa kutekeleza malengo yake ikiwemo kuanzisha mfumo wa kudhibiti madhara yatokanayo na matumizi ya dawa, chanjo na vifaa tiba kwa watumiaji.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Dkt.Vivian Wonanji
Huduma : Kaimu Meneja TMDA Kanda ya kaskazini
Mahali :ARUSHA
Mamlaka : TMDA
Contact : +255 762 55 36 13
No comments:
Post a Comment